2012
Mabinti katika Ufalme Wangu
Machi 2012


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Mechi 2012

Mabinti katika Ufalme Wangu

Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Imani, Familia, Usaidizi

Sisi tu mabinti wa Baba yetu aliye Mbinguni. Yeye anatujua sisi, anatupenda sisi na ana mpango kwetu sisi. Sehemu ya mpango huu inajumuisha kuja dunia ili kujifunza kuchagua mema badala ya maovu. Tunapochagua kuziweka amri za Mungu, tunamhesimu Yeye na kutambua utambulisho wetu kama mabinti wa Mungu. Muungano wa Usaidizi wa kina Mama unatusaidia kukumbuka urithi wetu mtakatifu.

Muungano wa Usaidizi wa kina Mama na historia yake hutuimarisha na kutuhimili. Julie B. Beck, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama, alisema: “Kama mabinti wa Mungu, mnajitayarisha kwa vyeo vya milele, na kila mmoja wenu ana utambulisho wa kike, asilia, na majukumu. Ufanisi wa familia, jamii, Kanisa hili, na mpango wa thamani wa wokovu unategemea uaminifu wenu. [Baba yetu wa Mbinguni] alidhamiria Muungano wa Usaidizi wa kina mama kusaidia kujenga watu Wake na kuwatayarisha kwa baraka za hekalu. Yeye aliasisi [Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama] kulinganisha mabinti Zake na kazi Yake na kupangia usaidizi wao katika kujenga ufalme Wake na kuimarisha nyumba za Sayuni.”1

Baba yetu aliye Mbinguni ametupatia sisi kazi mahususi ya kujenga ufalme Wake. Yeye pia ametubariki na vipawa vya kiroho tunavyohitaji kukamilisha kazi hii mahususi. Kupitia Muungano wa Usaidizi wa kina Mama, tuna nafasi za kutumia vipawa vyetu ili kuimarisha familia, kuwasaidia wale walio na mahitaji, na kujifunza jinsi ya kuishi kama wanafunzi wa Yesu Kristo.

Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alisema kuhusu uanafunzi: “Kwa kutembea kwa uvumilivu katika mapito ya uanafunzi, tunaonyesha kwetu wenyewe kipimo cha imani yetu na kupendelea kwetu kufanya mapenzi ya Mungu badala ya mapenzi yetu.”2

Acha tukumbuke sisi tu mabinti wa Mungu na tunajitahidi kuishi kama wanafunzi Wake. Tunapofanya hivyo, tutasaidia kujenga ufalme wa Mungu hapa ulimwenguni na kuwa wastahiki kurudi katika uwepo Wake.

Kutoka kwa Maandiko

Zakaria 2:10; Mafundisho na Maagano 25:1, 10, 16;138:38–39, 56; “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” Liahona na Ensign, Nov. 2010, 129)

Kutoka kwa Historia Yetu

Tarehe 28 Aprili 1842, Nabii Joseph Smith aliwaambia kina dada katika Muungano wa Usaidizi wa kina mama: “Nyinyi sasa mmewekwa katika hali ambayo kwayo mnaweza kutenda kulingana na huruma ambao Mungu ameupanda ndani [yenu] Ikiwa utaiishi kustahili heshima zako, malaika hawawezi kuzuiliwa kuwa washiriki wako.”3

Kutambua uwezo wa Muungano wa Usaidizi wa kina mama wa kuwahudumia wengine na kuwasaidia watu kuongezea imani, Zina D. H. Young, Rais mkuu wa tatu wa Muungano wa Usaidizi wa kima mama, aliwaahidi kina dada mnamo 1893, “Kama mtachimba ndani ya mioyo yenu wenyewe mtapata, kwa msaada wa Roho wa Bwana, lulu ya thamani kuu, ushuhuda wa kazi hii.”4

Muhtasari

  1. Julie B. Beck, “‘Daughters in My Kingdom’: The History and Work of Relief Society,” Liahona Nov. 2010, 112, 114.

  2. Dieter F. Uchtdorf, “The Way of the Disciple,” Liahona, May 2009, 76.

  3. Joseph Smith, katika History of the Church, 4:605.

  4. Zina D. H. Young, “How I Gained My Testimony of the Truth,” Young Woman’s Journal, Apr. 1893, 319.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Nawezaje kuwasaidia kina dada zangu kufikia kiwango chao kama mabinti wa Mungu?

  2. Nawezaje kutumia maishani mwangu ushauri na maonyo yaliyopatiwa wanawake katika Mafundisho na Maagano 25?