2012
Kuonyesha Uanafunzi Wetu kupitia Upendo na Huduma
Julai 2012


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Julai 2012

Kuonyesha Uanafunzi Wetu kupitia Upendo na Huduma

Kwa maombi soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Imani, Familia, Usaidizi

Maishani mwake mwote, Yesu Kristo alionyesha upendo Wake kwa wengine kwa kuwahudumia. Alisema, “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (John 13:35). Aliweka mfano na anataka sisi “tuwasaidia wale wanaohitaji usaidizi wenu” (Mosia 4:16). Yeye anawaita wanafunzi Wake kufanya kazi pamoja na Yeye katika huduma Yake, akiwapatia nafasi ya kuwahudumia wengine na kuwa zaidi kama Yeye.1

Huduma yetu kama waalimu watembelezi watafanana na huduma ya Mwokozi wetu tunapoonyesha upendo wetu kwa wale tunaowafunza kwa kufanya yafuatayo:2

  • Kumbuka majina yao na majina ya wanafamilia wao na kujifahamishana nao.

  • Kuwapenda bila kuwahukumu wao.

  • Watunze na kuimarisha imani yao “mmoja mmoja,” kama Mwokozi alivyofanya (3 Nephi 11:15).

  • Endeleza urafiki wa uaminifu nao na uwatembelee katika nyumba zao na kwengineko.

  • Mjali kila dada. Kumbuka siku za kuzaliwa, kufuzu, harusi, ubatizo, au nyakati zingine zilizo na maana kwake.

  • Watafute washiriki wapya na wale wasioshiriki kikamilifu.

  • Watafute walio wapweke au wanaohitaji faraja.

Kutoka kwa Maandiko

3 Nefi 11; Moroni 6:4; Mafundisho na Maagano 20:47

Kutoka kwa Historia Yetu

“Agano Jipya lina taarifa za wanawake, waliotajwa majina, na wale wasiotajwa, waliofanya imani katika Yesu Kristo. Hao wanawake wamekuwa mfano wa uanafunzi. [Wao] waliandamana na Yesu na Mitume Wake Kumi na Wawili. Walimpatia mali zao kwa kusaidia huduma Yake. Baada ya kufa na kufufuka Kwake, [wao] waliendelea kuwa wanafunzi waaminifu”3

Paulo aliandika juu ya mwanamke mmoja aliyeitwa Fibi, ambaye alikuwa “mtumishi wa kanisa” (Warumi 16:1). Yeye aliwaomba watu “wamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu: kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi” (Warumi 16:2). “Aina ya huduma iliyotolewa na Fibi na wanawake wengine wakuu katika Agano Jipya inaendelea leo na washiriki wa uongozi—wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, waalimu watembelezi, kina mama, na wengine—wanaotenda kama waauni au wasaidizi, wa wengi.”4

Muhtasari

  1. Ona Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 105.

  2. Ona Handbook 2 2: Administering the Church (2010), 3.2.3.

  3. Daughters in My Kingdom, 3.

  4. Daughters in My Kingdom, 6.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Ninaongezea uwezo wangu wa kuwatunza wengine vipi?

  2. Ninafanya nini kuhakikisha kwamba kina dada ninaotunza wanajua kwamba nawapenda?