2014
Viungo vya Upendo
Februari 2014


Watoto

Viungo vya Upendo

Wezesha mtu mzima akusaidie kukata vipande 28 nyembamba vya karatasi, kila moja takribani inchi 1 (2.5cm) kwa upana na takribani inchi 8 (20cm) kwa urefu. Kila siku mwezi huu, tenda kitendo cha huduma ili kuonyesha upendo wako kwa mtu flani. Unaweza kuwasaidia wazazi wako kusafisha nyumba yenu ama kuandika barua ya wema kwa jirani.

Andika jinsi ulivyohudumu kila siku kwenye kipande kimoja cha karatasi yako, kisha unganisha vipande pamoja ili kutengeneza duara. Unaweza kuunganisha duara zako kwa kuweka ukingo mmoja wa kipande kipya cha karatasi kupitia duara kutoka siku iliyopita kabla hujaunganisha kingo za kipande kipya pamoja. Tazama viungo vyako vya upendo vikikua! Unaweza hata kuendelea kuongezea kwa mfuatano wako wa huduma baada ya Februari kuisha.