2014
Mtumikie Bwana kwa Upendo
Februari 2014


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Februari 2014

Mtumikie Bwana kwa Upendo

Picha
Rais Thomas S. Monson

Bwana Yesu Kristo alifundisha, “Kwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha” (Luka 9:24).

“Ninaamini” alisema Rais Thomas S. Monson, “Mwokozi anatuambia kwamba isipokuwa tujipoteze katika utumishi kwa wengine, kuna kusudi dogo kwa maisha yetu wenyewe. Wale wanaoishi tu kwa ajili ya wao wenyewe hatimaye hunyauka na kistiari hupoteza maisha yao, ilhali wale wanaojitoa katika utumishi kwa wengine hukua na kustawi —na hakika huokoa maisha yao.”1

Katika dondoo ifuatayo kutoka kwa huduma ya Rais Monson, anawakumbusha Watakatifu wa Siku za Mwisho kwamba wao ni mikono ya Bwana na kwamba baraka za milele zinawangoja wale ambao kwa imani wanawatumikia wengine.

Huduma katika Hekalu.

“Huduma kuu hutolewa tunapofanya ibada tukufu kwa niaba ya wengine ambao wameaga. Katika matukio mengi hawatujui wale tunaowafanyia kazi. Hatutarajii shukrani, wala hatuna uhakika kwamba watapokea kile ambacho tunachotoa. Lakini, tunahudumu, na katika mwelekeo huo tunapokea kile ambacho huja si kwa juhudi zingine: kwa kweli tunakuwa waokozi kwenye Mlima Sayuni. Kama vile Mwokozi wetu alivyotoa maisha Yake kama dhabihu kwa niaba yetu, hivyo sisi, katika kipimo kidogo, tunafanya vile vile tunapofanya kazi kwa niaba ya wengine katika hekalu kwa wale ambao hawana namna ya kuendelea mbele isipokuwa jambo lifanywe kwa niaba yao na wale wetu walio hapa duniani.2

Sisi ni Mikono ya Bwana

“Akina ndugu na dada zangu, tumezingirwa na wale wanaohitaji ya usikivu wetu, himizo letu, msaada wetu, faraja yetu, ukarimu wetu—wawe wana familia, marafiki, jamaa, ama wageni. Sisi ni mikono ya Bwana hapa duniani, tukiwa na jukumu la kuwatumikia na kuwainua watoto Wake. Yeye anamtegemea kila mmoja wetu …

“Huduma hiyo ambayo kwayo kila mmoja wetu ameitwa ni huduma ya Bwana Yesu Kristo.”3

Kuhudumu katika Kivuli cha Bwana

Katika Ulimwengu Mpya, Bwana aliyefufuka alitangaza, “Mnajua vitu ambavyo mnahitajika kufanya katika Kanisa langu, kwani vitendo mmeniona nikifanya, hivyo pia mtafanya; kwani yale ambayo mmeniona nikifanya hata hivyo nyinyi mtafanya.” [3 Nefi 27:21].

“Tunawabariki wengine tunapohudumu katika kivuli cha “Yesu wa Nazareti … aliyezunguka huko na huko akitenda kazi njema.” [Matendo ya Mitume 10:38]. Mungu atubariki ili tupate furaha katika kumtumikia Baba yetu aliye Mbinguni tunapowatumikia watoto Wake duniani.”4

Haja ya Kuhudumu

“Tunahitaji kupewa fursa ya kuhudumu. Kwa wale washiriki walioteleza kutoka kwa ushiriki kamili ama wanaojizuia ama kubaki wakiwa hawajaamua, tunaweza kutafuta kwa maombi njia fulani ya kuwafikia. Kuwauliza wahudumu katika kiwango fulani huenda ikawa motisha wanaohitaji ili kurudi katika ushiriki kamilifu. Lakini wale viongozi ambao wanaweza kusaidia katika suala hili mara nyingi huwa wanasita kufanya hivyo. Tunahitaji kukumbuka kwamba watu wanaweza kubadilika. Wanaweza kuweka nyuma yao mazoea mabaya. Wanaweza kutubu dhambi. Wanaweza kuhimili ukuhani kwa ustahiki. Na wanaweza kumtumikia Bwana kwa bidii.”5

Je, Tunafanya Yote ambayo Tunapaswa Tufanye?

“Dunia inahitaji msaada wetu. Je, tunafanya yote ambayo tunapaswa tufanye? Je, tunakumbuka maneno ya Rais John Taylor: “Msipokuza miito yenu, Mungu atawawajibisha kwa wale ambao mngewaokoa kama mngefanya jukumu lenu.’? Teachings of Presidents of the Church: John Taylor (2001), 164]. Kuna miguu ya kuimarisha, mikono ya kushikilia, akili za kuhimiza, moyo wa kushawishi, na nafsi za kuokoa. Baraka za milele zinakungoja. Yenu ni fursa ya kutokuwa watazamaji lakini washiriki kwenye jukwa la huduma.”6

Muhtasari

  1. “Je, Nimemfanyia nini Mtu Leo?” Liahona, Nov. 2009, 85.

  2. “Hadi Tutakapokutana Tena,” Liahona, Mei 2009, 113–14.

  3. “Je, Nimemfanyia nini Mtu Leo?” 86, 87.

  4. “Wito wa Mwokozi Kuhudumu,” Liahona, Aug. 2012, 5.

  5. “Ona Wengine Kama Vile Wanaweza Kuwa,” Liahona, Nov. 2012, 68.

  6. “Tayari na Mstahiki Kuhudumu,” Liahona, Mei 2012, 69.

  7. Teaching, No Greater Call: A Resource Guide for Gospel Teaching (1999), 12

Kufundisha kutoka kwenye Ujumbe huu

“Ukiwa una upendo kama wa Kristo, utakuwa tayari zaidi kufundisha injili. Utapata ushawishi wa kuwasaidia wengine kumjua Mwokozi na kumfuata Yeye.”7Zingatia kuomba kwa ongezeko la hisani kwa wale unaowatembelea. Unapokuza upendo kama wa Kristo kwa ajili yao, utakuwa na uwezo bora zaidi kuwahudumia kwa njia za maana wote, Bwana na wale unaowafundisha.