2014
Je, Naweza Kufurahia Uorodheshaji?
June 2014


Vijana

Je, Naweza Kufurahia Uorodheshaji?

Mtunzi anaishi Veracruz, Mexico.

Nilishiriki katika lengo letu la kigingi la kuorodhesha majina 50,000. Mara ya kwanza ilikuwa vigumu. Mara kadhaa kundi nililopakuwa lilikuwa na hati ngumu, na wakati mwingine nilitaka kuirudisha na kutoa nyingine tofauti. Lakini nilitambua kwamba kama kila mtu alifikiri hivyo, makundi hayo yangeachwa hadi mwisho. Ningewazia mistari mingi ya watu wakisubiri katika ulimwengu wa roho, na nikaamua kuendelea kujaribu kusoma yale majina na kuyanakili bila kufanya makosa.

Nilijifunza kuwa na upendo kwa watu wale. Nilielewa kwamba hakika walihitaji msaada, na sisi pia tulihitaji msaada kutoka kwao. Nilikuja kuelewa vyema zaidi kwamba mpango kamili wa Baba wa Mbinguni unajali kila mtu. Tunapofuata maongozi na maelekezo ya viongozi Wake wateule, tutashuhudia huruma Yake na upendo Wake usio na mwisho.

Uorodheshaji umekuwa tukio la kupendeza kwangu. Nilijifunza kuthamini na kupenda mambo mengi kuhusu historia ya familia. Pia nilipata karama ya thamani kubwa kutoka kwa Bwana wetu kwa kutii kitu rahisi kama kushiriki katika uorodheshaji.