2014
Jueni Hadithi Zenu
June 2014


Watoto

Jueni Hadithi Zenu

Wazazi wenu na mababu zenu wamekuwa na matukio mengi ya ajabu — mengine ambayo hamjui kuyahusu! Baadhi ya hadithi zao zitawafanya mcheke, na zinaweza kuwasaidia kuwa na imani kwa Baba wa Mbinguni. Lakini hata watu wazima huona haya wakati mwingine. Tumia maswali haya ili kuwasaidia kukumbuka baadhi ya hadithi zao wazipendazo na uandike au uchore picha za majibu yao.

  1. Niambie kuhusu kumbukumbu zako tatu za furaha zaidi.

  2. Ni wakati gani uliokuwa wa aibu zaidi kwako?

  3. Niambie kuhusu siku nilipozaliwa.

  4. Ulipendelea kufanya nini ulipokuwa mtoto?

  5. Uliupata aje ushuhuda wako wa injili?