2016
Matendo ambayo Yanelekeza kwenye Furaha
Januari 2016


Vijana

Matendo ambayo Yanaelekeza kwenye Furaha

Rais Eyring anafundisha kwamba “furaha tunayowatakia wapendwa wetu hutegemea maamuzi yao.”

Unaweza kusoma kuhusu athari ambazo chaguo zinaweza kuleta kutokana na mifano ya Nefi, Lamani na Lemueli. Lamani na Lemueli walinung’unika na hawakutaka kushika amri (ona 1 Nefi 2:12). Matokeo yake, wao na uzao wao ulilaaniwa na kukatiliwa mbali kutoka kwenye uwepo wa Bwana (ona 2 Nefi 5:20–24). Nefi alichagua kutii amri (ona 1 Nefi 3:7), na kwa sababu hiyo, yeye na watu wake waliishi kwa furaha (2 Nefi 5:27).

Unaweza chagua kuwa mwema na kuwa na furaha. Lakini watu wanaokuzunguka labda bado wafanya chaguzi mbaya ambazo zinaelekeza kwenye taabu na usumbufu. Hali kwamba hayo maamuzi ni yao, mfano wako unaweza kushawishi chaguo zao kutenda mema. Je! Chaguo unazofanya zinaweza kuwaletea furaha wengine vipi? Jadili na familia yako njia tofauti mnazoweza kuleta ushawishi chanya kwa wale walio karibu nanyi na kuwasaidia kuhisi furaha.