2016
Changamoto - za ukarimu
Januari 2016


Watoto

Jaribu la ukarimu

Wakati Yesu Kristo alipotembelea watu katika Amerika, Yeye aliwafundisha kupendana mmoja na mwingine na kuwa wakarimu. Je! Unaweza kufanya nini ili kumfuata Yesu Kristo na kuwapenda wengine? Haya ni baadhi ya mawazo: Utie tiki kila Changamoto unapoendelea.

  • □ Ninaweza kumkumbatia mtu mwenye huzuni.

  • □ Ninaweza kumhudumia mtu fulani kwa siri!

  • □ Ninaweza kusoma na kutazama hotuba ya mkutano mkuu kuhusu kuwa mkarimu.

  • □ Ninaweza kuimba wimbo wa Msingi kwa familia.

  • □ Ninaweza kutabasamu kwa mtu anayeonekana kuwa mpweke.

  • □ Ninaweza __________________________________________.

  • □ Ninaweza __________________________________________.