2016
Msingi kwa ajili ya Ushuhuda Wangu
Februari 2016


Vijana

Msingi wa Ushuhuda Wangu

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Nilipokuwa na miaka 16, rafiki yangu alifika nyumbani kwetu pamoja na wamisionari. Katika muda wa mwezi mmoja wa mazungumzo yetu ya kwanza, maswali yangu yote yalikuwa yemejibiwa bayana. Nilihisi Roho Mtakatifu akishuhudia ukweli wa ujumbe kuhusu Urejesho. Ilikuwa tofauti na kitu chochote nilichowahi kuhisi, na nilifahamu kuwa yote yalikuwa ya kweli.

Hata hivyo, nilikataliwa na kupata upinzani zaidi kuliko mbeleni. Nilihisi upweke, uchovu, na kuchanganyikiwa. Ikiwa nilikuwa nafanya vyema, kwa nini nilikuwa nakumbana na shida nyingi? Sikuelewa jinsi majaribio yangu yalikuwa kwa ajili ya manufaa yangu. Wamisionari walinifunza kufunga na kuomba, hata katikati mwa siku ya shule. Wakati ambapo mambo yalikuwa magumu zaidi niliomba na papo hapo nilihisi faraja ya Roho.

Wiki ya kubatizwa kwangu ilikuwa na majaribio mengi. Bosi wangu alitishia kunifuta kazi kama ningehudhuria ubatizo wangu badala ya kwenda kumsimamia mtu fulani ambaye hakuwa kazini, niliishia hospitalini na mawe kwenye figo, na wazazi wangu waliniambia nihame nyumbani. Na mambo mengi mno ambayo sikuwa na uwezo wa kufanya, kile ambacho nilikuwa na uwezo wa kufanya ilikuwa ni kumgeukia Bwana.

Kila moja ya majaribio hayo yaligeuka kuwa ya manufaa kwangu. Yalinisaidia kujifunza kuhusu mafundisho ya injili, ambayo yalinipa msingi wa ushuhuda wangu.