2016
Kutua Salama Kwenye Ghasia
Februari 2016


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Februari 2016

Kutua Salama katika Ghasia

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

Si muda mrefu uliopita mke wangu, Harriet, pamoja nami tulikuwa katika kiwanja cha ndege tukitazama ndege kubwa zikitua. Ilikuwa siku yenye upepo mwingi, na dhoruba kali ya upepo ilipiga dhidi ya ndege iliyokuwa ikikaribia kutua, na kusababisha kila moja kutetemeka na kuwa na wasiwasi wakati ikikaribia.

Tulipokuwa tukiangalia kwa makini mapambano kati ya ulimwengu na mashine, mawazo yangu yalirejelea mafunzo yangu ya urubani na kanuni nilizojifunza huko—na baadaye nikawafundisha marubani wengine wakati wa mafunzo yao.

”Usije ukapambana na vidhibiti wakati wa ghasia“, Nilikuwa nikiwaambia. “Kuwa mtulivu; usijibu kupita kiasi. Lenga macho yako kwenye laini ya katikati mwa njia ya ndege. Ikiwa utakosea njia yako ya kutua, fanya marekebisho papohapo kwa kipimo. Kuwa na imani kwenye uwezo wa ndege yako. Vumilia hadi ghasia ipite.“

Marubani walio na tajriba wanaelewa kuwa hawawezi kila mara kuzuia kila kitu ambacho hufanyika karibu na wao. Hawawezi tu kuzima ghasia. Hawawezi kuifanya mvua au theluji kupotea. Hawawezi kusababisha upepo uwache kupuliza au ubadilishe mwelekeo.

Lakini pia wanaelewa kuwa ni makosa kuogopa ghasia au upepo mkali—na hasa kufadhaishwa nazo. Njia ya kutua salama wakati hali sio nzuri sana ni kukaa imara kwenye njia ya kutua kikamilifu vilivyo.

Nilipokuwa nikitazama ndege moja baada ya nyingine ikitua na kukumbuka kanuni nilizojifunza kuanzia miaka yangu kama rubani, niliwaza ikiwa hapakuwepo cha kujifunza kutokana na haya katika maisha yetu ya kila siku.

Hatuwezi kila siku kudhibiti dhoruba ambazo maisha huleta njiani mwetu. Mara nyingine, mambo kwa kawaida hayaendi jinsi tunavyotaka. Tunaweza kuwa na wasiwasi na kuhisi tunapeperushwa na ghasia za masikitiko, wasiwasi, hofu, huzuni, au mfadhaiko.

Wakati kama huo, ni rahisi kuchanganyikiwa na kila kitu kinachoenda kombo na kufanya shida zetu kuwa mawazoni mwetu. Majaribu ni kuzingatia majaribio ambayo tunakumbana nayo badala ya Mwokozi na ushuhuda wetu wa kweli.

Lakini hiyo si njia muwafaka ya kabiliaana na shida zinazotukumba maishani.

Kama ilivyo kwa rubani mwenye tajriba halengi kwenye dhoruba lakini laini ya katikati mwa barabara ya ndege na mahali sawa pa kutua, hivyo basi nasi lazima tulenge katikati mwa imani yetu—Mwokozi wetu, injili Yake, na mpango wa Baba yetu wa Mbinguni—na lengo letu la mwisho—kurudi salama hadi mbinguni mwisho wa safari yetu. Tunafaa kumuamini Mungu na kufanya kuwa kwenye njia ya uanafunzi lengo la jitihadi zetu. Tunafaa kulenga macho yetu, moyo, na akili kwa kuishi jinsi tunajua tunatakikana.

Tukionyesha imani yetu na kuwa tunamuamini Baba wa Mbinguni kwa kutii kwa furaha amri zake itatuletea furaha na ufalme. Na tukibaki kwenye njia, tutaweza kupita kwenye ghasia zozote—hata zikionekana zenye nguvu kiasi gani—na kurudi salama nyumbani kwetu mbinguni.

Iwe anga karibu nasi ni wazi au imejaa mawingu yenye kutisha, kama wanafunzi wake Yesu Kristo, tunatafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, tukifahamu kwamba tukifanya hivyo, vitu vingine vyote tunavyohitaji hatimaye atatupa (Ona Mathayo 6:33).

Funzo muhimu katika maisha lilioje!

Tunavyozidi kulenga shida zetu, mapambano yetu, wasiwasi wetu, na hofu yetu, ndivyo mambo yanavyozidi kuwa magumu. Lakini tunavyozidi kulenga mwisho wa safari yetu ya mbinguni na furaha ya kufuata njia ya mwanafunzi—kumpenda Mungu, kuhudumia jirani yako—ndivyo kunazidi kuwa na uwezekano wa kukabiliana na nyakati za shida na ghasia.

Marafiki wapendwa, bila kujali upepo wa maisha yetu ya sasa uwe mkali kiasi gani na kutoa sauti kali karibu nasi, injili ya Yesu Kristo daima itakuwa na njia bora zaidi ya kutua salama katika ufalme wa Baba wa Mbinguni.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Raisi Uchtdorf anatushauri kuwa “amini Mungu na kaa kwenye njia ya uanafunzi lengo la jitihadi zetu.” Zingatia kuwauliza wale unaowafundisha jinsi ambavyo wamebaki wakilenga “mwisho wa safari yetu mbinguni na furaha ya kufuata njia ya uanafunzi” wakati ambao wamepitia majaribio. Unaweza kuwaalika kufikiria kuhusu njia ambazo wanaweza kulenga ushuhuda wao na Kristo wakati wanapitia kwenye shida na kwa maombi waamue jinsi ya kutekeleza mojawapo au zaidi ya malengo hayo katika maisha yao.