2016
Kuumbwa katika Mfano wa Mungu.
Machi 2016


Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Machi 2016

Kuumbwa katika Mfano wa Mungu.

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Je! Kuelewa “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” kunawezaje kuongeza imani yako katika Mungu na kuwabariki wale unaowachunga kwa njia ya ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.

Picha
Nembo ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; 

“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwanzo 1:26–27).

Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, na Alituumba kwa mfano Wake. Kuhusu ukweli huu, Rais Thomas S. Monson alisema: “Mungu Baba yetu ana msikio ambayo kwayo anasikia maombi yetu. Yeye ana macho ambayo kwayo anaona matendo yetu. Yeye ana mdomo ambao kwao anatuongelesha. Yeye ana moyo ambao kwao anahisi huruma na upendo. Yeye ni halisi. Yeye yu hai. Sisi watoto wa Mungu, walioumbwa kwa mfano Wake. Tunafanana naye, Naye anafanana nasi.”1

“Watakatifu wa Siku za Mwisho wanawaona watu wote kama watoto wa Mungu katika hali zote na ukamilifu; wanamchukulia kila mtu kuwa na uungu katika uasili, hasili, na uwezo.”2 Kila mmoja ni “mwana ama binti mpendwa wa kiroho wa wazazi wa mbinguni.”2

“[Nabii] Joseph Smith pia alijifunza kwamba Mungu anataka watoto Wake wapokee aina hiyo hiyo ya hali iliyoinuliwa ambayo ndivyo alivyo.”4 Kama Mungu alivyosema, “Kwa maana tazama, hii ndiyo kazi yangu na utukufu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).

Maandiko ya Ziada

Mwanzo 1:26–27; 1 Wakorintho 3:17; Mafundisho na Maagano 130:1

Kutoka katika Maandiko

Kaka wa Yaredi katika Kitabu cha Mormoni akitafuta njia ya kuangaza mashua nane ambazo zilisanifiwa kuwabeba Wayaredi kuvuka maji hata nchi ya ahadi. “Alichoma mawe kumi na sita madogo kutoka kwa mwamba” na kuomba kwamba Mungu “ayaguse mawe haya” kwa kidole Chake “kwani yaweze kung’aa katika giza.” Na Mungu “alinyoosha mbele mkono wake na kugusa yale mawe moja moja.” Na pazia lilitolewa machoni mwa kaka ya Yaredi, na “akaona kidole cha Bwana; na kilikuwa kama kidole cha mtu…. 

Na Bwana akamwambia: “Utaamini maneno ambayo nitayasema?”

“Naye akajibu: Ndio, Bwana.”

Na “Bwana kisha akajionyesha kwa [kaka ya Yaredi]” na kusema, “Je, unaona kwamba uliumbwa kwa mfano wangu? Ndio, hata watu wote waliumbwa katika mwanzo kwa jinsi ya kama maumbile yangu.” (Ona Etheri 3:1–17.)

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, I Know That My Redeemer Lives, in Conference Report, Apr. 1966, 63.

  2. Gospel Topics, Becoming Like God, topics.lds.org; ona pia Musa 7:31–37.

  3. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu, Liahona, Nov. 2010, 129.

  4. Gospel Topics, Becoming Like God, topics.lds.org; ona pia Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 221.

Zingatia Hili

Ni kwa jinsi gani kujua kwamba kila mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu kutatusaidia sisi katika mahusiano yetu na wengine?