2018
Toba ni Kipawa
January 2018


Watoto

Toba ni Kipawa

Kipawa cha toba si kipawa ambacho unaweza kukiona au kukishika. Badala yake, ni kipawa ambacho unaweza kukihisi. Hii inamaanisha kwamba tunapofanya chaguo baya, tunaweza kutubu na kuhisi amani na furaha tena.

Baba wa Mbinguni na Yesu daima watatusaidia kutubu. Chora picha ya kuendana na kila hatua tofauti ya toba.

Tunahisi kujuta.

Tunasali kwa Baba wa Mbinguni, kumwambia Yeye kile ambacho kimetokea, tunamwomba msaada Wake ili kufanya chaguzi bora zaidi wakati ujao.

Tunaomba msamaha na kujaribu kurekebisha.

Tunaweza kuhisi amani na kujua kwamba tumesamehewa.