2018
Amua Kutubu
January 2018


Vijana

Amua Kutubu

Rais Monson anaeleza kwamba “Ni jukumu letu kuinuka kutoka uhafifu hadi ukamilifu, kutokana na ushinde hadi kufaulu. Kazi yetu ni kuwa bora zaidi wenyewe.” Watu wengi wanatenga Januari kwa ajili ya kuweka malengo na maazimio: kutabasamu zaidi, kula lishe ya afya zaidi, au kujifunza ujuzi mpya. Hali malengo haya yanaweza kukusaidia kubadilika kuwa bora, njia bora ya kubadilika ni kupitia toba.

Ingawa toba inaweza kuwa ngumu, ni kipawa! Tunapomtegemea Yesu Kristo kwa kutubu dhambi zetu, tunaweza kukua na kuendelea. Rais Monson alisema, “Muhimu katika mpango [wa wokovu] ni Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Bila dhabihu Yake ya upatanisho, yote yangepotea. Kupitia toba, unaweza kuoshwa dhambi zako na kuendelea kuwa zaidi kama Yeye.

Fikiria kitu ambacho kinaweza kukuzuia kuwa kama Mwokozi. Ni lugha yako? Ni jinsi unavyowatendea marafiki zako au familia? Baada ya kufikiria kile unachoweza kuboresha, sali kwa Baba wa Mbinguni na uonyeshe hamu ya kutaka kubadilika. Kumbuka kwamba kupitia nguvu za Upatanisho Wake, Yesu Kristo anaweza kukusaidia kushinda udhaifu wako. Kama vile Rais Monson alivyofundisha, “Kipawa cha toba, kinachotolewa na Mwokozi wetu, hutuwezesha kurekebisha njia yetu.”