2023
Nyenzo kwa ajili ya Vijana na Watoto
Februari 2023


“Nyenzo kwa ajili ya Vijana na watoto,” Liahona, Feb. 2023.

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Liahona, Februari 2023

Nyenzo kwa ajili ya Vijana na Watoto

Picha
wazazi wakisoma maandiko pamoja na mwana wao

Wazazi wana jukumu la msingi la kuwafundisha watoto wao kuhusu Yesu Kristo na injili Yake. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lina taasisi, programu na nyezo nyinginezo ili kuwasaidia wazazi katika juhudi zao. Kwa pamoja, wazazi, viongozi wa Kanisa na marafiki wanaweza kuwasaidia watoto wote na vijana kuja kwa Kristo.

Picha
Watoto wa Msingi

Picha na Ben Johnson

Msingi

Msingi ni kikundi cha Kanisa kwa ajili ya watoto wa umri wa miezi 18 hadi miaka 11. Katika Msingi, watoto wanajifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake kupitia masomo, muziki na shughuli mbalimbali. Msingi inaweza kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Mungu kwao.

Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana

Katika mwezi wa Januari ya mwaka ambao watoto wanafikisha miaka 12, wanahama kutoka Msingi kwenda ama kuingia katika akidi za Ukuhani wa Haruni (kwa wavulana) au madarasa ya Wasichana (kwa wasichana). Katika akidi zao na madarasa, vijana wanaendelea kuimarisha shuhuda zao na kuwatumikia wengine.

Picha
mikono ikichora picha

Programu ya Watoto na Vijana

Katika ujana Wake, Yesu Kristo alizidi kukua “katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu” (Luka 2:52). Programu ya Watoto na Vijana huwasaidia waumini wachanga wa Kanisa kufuata mfano wa Yesu Kristo. Wanajifunza na kukua katika nyanja zote za maisha yao—kiroho, kijamii, kimwili na kiakil.

Magazeti ya Kanisa

Gazeti la Kanisa kwa ajili ya watoto ni gazeti la Rafiki. Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ni gazeti mahsusi kwa vijana. Magazeti haya yanajumuisha hadithi, mafundisho na shughuli zilizoandikwa mahsusi kwa ajili ya watoto na vijana wadogo.

Picha
jalada la kitabu cha mwongozo katika lugha ya Kihispania

Kitabu cha Mwongozo cha Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana

Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi kinawafundisha vijana kuhusu kweli za injili. Kinawafundisha jinsi ya kufanya maamuzi ambayo yatawasaidia wao kumfuata Yesu Kristo. Pia kinajumuisha majibu kwa maswali ambayo vijana wanaweza kuwa nayo kuhusu jinsi ya kuishi injili.

Maktaba ya Injili

Maktaba ya Injili inazo nyenzo za kidijitali nyingi, ikijumuisha video, muziki, hadithi za maandiko matakatifu na shughuli. Pia inajumuisha nyenzo za kuwasaidia wazazi na viongozi kufundisha kanuni za injili. Nyenzo hizi zinapatikana katika Maktaba ya Injili kwenye ChurchofJesusChrist.org na katika aplikesheni ya Gospel Library.

Mikutano ya KNV

Mwanzoni mwa mwaka wanaofikisha umri wa miaka 14, vijana wanaalikwa kuhudhuria makongamano ya Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (KNV). Matukio haya yanajumuisha shughuli na madarasa ambayo yanasaidia kuimarisha imani katika Yesu Kristo na kuwasaidia vijana kukua kiroho, kijamii, kimwili na kiakili.