2023
Mfungulie Roho Mtakatifu Moyo Wako
Aprili 2023


“Mfungulie Roho Mtakatifu Moyo Wako,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Apr. 2023.

Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Aprili 2023

Mfungulie Roho Mtakatifu Moyo Wako

Katika msimu huu wa Pasaka, ninamshukuru Baba yetu wa Mbinguni kwa Zawadi ya Mwanawe Mpendwa, ambaye alikuja kwa hiari duniani kuwa Mkombozi wetu. Nina shukrani kujua kwamba alifanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka katika ufufuko. Kila siku ninabarikwa kujua kwamba, kwa sababu ya Upatanisho Wake, siku moja ninaweza kufufuka na kuishi milele katika familia yenye upendo.

Ninajua vitu hivyo kwa njia pekee ambayo kila mmoja wetu anaweza kujua. Roho Mtakatifu amezungumza akilini mwangu na moyoni mwangu kwamba ni vya kweli—si mara moja tu bali kila mara.

Tuna ahadi ya thamani sana ya Roho Mtakatifu kama mwenzi. Jukumu letu ni kuchagua kufungua mioyo yetu ili tupokee maelekezo na faraja endelevu ya kiroho kupitia Roho Mtakatifu katika maisha yote.

Picha
ua

Vielelezo na Emily E. Jones

Uchaguzi wa kwanza ni kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu.

Picha
mikono ya sala

Wa pili ni kusali kwa imani kupitia Bwana Yesu Kristo.

Picha
dira

Wa tatu ni kutii kwa usahihi.

Picha
umbo la moyo

Na wa nne ni kusali ili kujua mahitaji na mioyo ya wengine na jinsi ya kuwasaidia kwa niaba ya Bwana.

Ninasali kwa moyo wangu wote kwamba mtaisikia sauti ya Roho, ambayo inatumwa kwenu kwa ukarimu. Na ninasali kwamba utaufungua moyo wako daima ili umpokee Roho kwamba uweze kuwa na shangwe ya kuwa na Roho pamoja nawe kama mwenzi wako daima.