2023
Yesu Anamrudishia Uhai Lazaro
Aprili 2023


“Yesu Anamrudishia Uhai Lazaro,” Rafiki, Apr. 2023, 46–47.

Jumbe za Kila Mwezi za Rafiki, Aprili 2023

Yesu Anamrudishia Uhai Lazaro

Picha
Yesu akiwa pamoja na Mariamu, Martha na Lazaro

Vielelezo na Apryl Stott

Mariamu na Martha walikuwa na kaka aliyeitwa Lazaro. Walikuwa marafiki wa Yesu Kristo.

Picha
Yesu akiwakumbatia Mariamu na Martha

Lazaro akawa mgonjwa sana. Punde, akafa. Mariamu na Martha walikuwa na huzuni. Yesu alipokuja, alilia pamoja nao.

Picha
Yesu akiwa amesimama kwenye kaburi la Lazaro

Kisha Yesu alienda pamoja nao kwenye kaburi la Lazaro. Akasema, “Lazaro, njoo huku nje.”

Picha
Yesu akimsaidia Lazaro atoke kaburini

Lazaro alisimama na kutembea kutoka kaburini. Alikuwa hai tena! Kwa sababu ya Yesu, sisi sote pia tutaishi tena!

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Yesu Kristo yu Hai

Picha
Ukurasa wa kupaka rangi wa mtoto akiwa ameshikilia picha ya Yesu

Kielelezo na Apryl Stott

Ni kwa jinsi gani unamkumbuka Yesu wakati wa Pasaka?