2023
Roho Mtakatifu Anaweza Kutusaidia
Juni 2023


“Roho Mtakatifu Anaweza Kutusaidia,” Liahona,, Juni 2023.

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Liahona, Juni 2023

Roho Mtakatifu Anaweza Kutusaidia

Picha
mtu amekaa na akitazama kuchomoza kwa jua

Roho Mtakatifu ni mshiriki wa tatu wa Uungu. Maandiko pia humwelezea Yeye kama Roho, Roho Mtakatifu au Mfariji. Tunapojifunza kusikiliza sauti Yake, Yeye atatushuhudia sisi juu ya Yesu Kristo na kutusaidia kujifunza kweli za injili.

Mshiriki wa Uungu

Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu ndio Uungu. Wanatupenda na wanafanya kazi katika umoja ili kukamilisha ule mpango wa wokovu. Ingawa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanayo miili ya nyama na mifupa; Roho Mtakatifu hana. Yeye ni roho.

Picha
picha ya Baba na Mwana kwenye kioo kilichopakwa rangi

Shahidi wa Baba na Mwana.

Roho Mtakatifu anashuhudia juu ya Baba na Mwana (2 Nefi 31:18). Hii humaanisha kwamba sisi tunaweza kupokea ushuhuda juu ya Baba Yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo kupitia Roho Mtakatifu.

Anashuhudia juu ya ukweli

Roho Mtakatifu anashuhuda juu ya ukweli wote. Yeye atatusaidia sisi kujua kwamba injili—ikijumlisha mpango wa wokovu, amri za Mungu, Urejesho, na Upatanisho wa Yesu Kristo—ni kweli. Yeye ataimarisha ushuhuda wetu tunapoendelea kusali, kushika amri, na kujifunza injili.

Picha
mkono umeshikilia dira

Hutuongoza na Kutulinda

Roho Mtakatifu anaweza kutuongoza katika maamuzi yetu na kutulinda kutokana na hatari ya kimwili na kiroho. Yeye atatusaidia kupata majibu ya maswali yetu kama tutasali na kujaribu kufanya kilicho sahihi. Yeye daima atatuongoza “kufanya mema” (Mafundisho na Maagano 11:12).

Hutufariji

Roho Mtakatifu wakati mwingine anaitwa kama “Mfariji” (Yohana 14:26). Yeye anaweza akatujaza “matumaini na upendo mkamilifu” (Moroni 8:26) tunapokuwa na mashaka, huzuni, au tunapokuwa waoga. Wakati Anapotusaidia kuhisi upendo wa Mungu, tunaweza kushinda kukatishwa tamaa na kuweza kuimarishwa katika majaribu yetu.

Kipawa cha Roho Mtakatifu

Baada ya kuwa tumebatizwa, tunapokea kipawa cha Roho Mtakatifu katika ibada inayoitwa uthibitisho. Mara tupokeapo kipawa hiki, ndipo tunapokuwa na ushirika wa kudumu wa Roho Mtakatifu ilimradi tunaendelea kuishi kwa uadilifu.

Picha
mwanamke akisoma maandiko

Kielelezo na J. Kirk Richards

Namna Tunavyomsikia Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu anawasiliana na watu katika njia tofauti. Hizi zinaweza kujumuisha njia za amani, hisia zenye kufariji au tambuzi kuhusu kitu gani cha kusema au kufanya. Tunaposali kwa ajili ya mwongozo na kusikiliza misukumo Yake, tunaweza kujua jinsi gani Yeye anaongea na sisi.