2023
Sakramenti ya Kwanza
Juni 2023


“Sakramenti ya Kwanza,” Rafiki,, Juni 2023, 46–47.

Jumbe za kila mwezi za gazeti la Rafiki, Juni 2023

Hadithi za Maandiko

Sakramenti ya Kwanza

Picha
Yesu amekaa mezani pamoja na Mitume Wake

Vielelezo na Apryl Stott

Kabla ya kufa, Yesu Kristo alikutana na Mitume Wake. Aliwapatia sakramenti.

Picha
Yesu akiwa ameshika mkate

Yesu alimega mkate na kuwapatia. Aliwaagiza waule ili kuwasaidia wao wakumbuke kwamba Yeye aliutoa uhai Wake kwa ajili yao.

Picha
Yesu akiwa ameshika kikombe

Kisha Yesu akawapa kikombe. Akawapa kutoka hicho. Kingewasaidia kumkumbuka Yeye pia.

Picha
Wakristo wa awali wakila sakramenti.

Hata baada ya Yesu kutokuwa pamoja na Mitume Wake, sakramenti iliwasaidia wao kumkumbuka Yeye. Waliweza kuhisi upendo Wake na kukumbuka kushika amri.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Ninaweza Kupokea Sakramenti

Picha
Mvulana akipokea sakramenti

Kielelezo na Apryl Stott

Ninapopokea sakramenti, ninaweza kumkumbuka Yesu na upendo Wake kwaangu.