2023
Neno la Mwisho: Tafuta Uelewa
Agosti 2023


“Tafuta Uelewa,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Agosti 2023.

Ujumbe wa kila Mwezi Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Agosti 2023

Tafuta Uelewa

Imetoholewa kutoka kwenye hotuba ya mkutano mkuu wa Aprili 2019.

Picha
mwanamke akiwa na taa ya mafuta

Vielelezo na Emily Jones

Lengo letu tunapotafuta uelewa wa injili ya Yesu Kristo lazima liwe ni kuongeza imani katika Mungu na mpango Wake mtakatifu wa furaha na katika Yesu Kristo na dhabihu Yake ya upatanisho na kufikia uongofu wa kudumu. Ongezeko la imani na uongofu wa aina hii vitatusaidia tufanye na tutunze maagano na Mungu, hivyo kuimarisha hamu yetu ya kumfuata Yesu na kuleta badiliko la kiroho la kweli ndani yetu. Badiliko hili litatuletea maisha yenye furaha zaidi, mafanikio, na afya bora na kutusaidia tudumishe mtazamo wa milele.

Picha
mvulana akisoma maandiko

Ili kufanikisha hili, tunahitaji kukaa katika Yesu Kristo kwa kuzama sisi wenyewe katika maandiko, tukiyafurahia, kujifunza mafundisho Yake, na kujitahidi kuishi kama Yeye alivyoishi. Ndipo hapo tutakuja kumjua Yeye na kuitambua sauti Yake, tukijua kwamba tunapokuja Kwake na kumwamini Yeye, kamwe hatutaona njaa wala kiu (ona Yohana 6:35).

Picha
mvulana akisali

Hilo halitokei kwa bahati. Kujizoeza sisi wenyewe kwenye ushawishi mkuu zaidi wa kiungu si jambo rahisi; kunahitaji kusali na kujifunza namna ya kuleta injili ya Yesu Kristo kwenye kiini cha maisha yetu.

Picha
msichana akigusa moyo wake

Ninatoa ushuhuda kwenu kwamba wakati kwa dhati, kwa moyo wote, kwa uimara, na kwa moyo wa kweli tunatafuta uelewa wa injili ya Yesu Kristo na kufundishana sisi kwa sisi kwa kusudi la dhati na chini ya uelekezi wa Roho, mafundisho haya yanaweza kubadili mioyo na kuchochea nia ya kuishi kulingana na kweli za Mungu.