2023
Wachungaji Wakimtembelea Mtoto Yesu
Desemba 2023


“Wachungaji Wakimtembelea Mtoto Yesu,” Rafiki, Des. 2023, 46–47.

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Desemba 2023

Wachungaji Wakimtembelea Mtoto Yesu

Picha
Alt text

Vielelezo na Apryl Stott

Usiku mmoja, malaika aliwatembelea wachungaji, kondemi. Malaika aliwaambia kwamba mtoto wa muhimu alikuwa amezaliwa. Jina lake lilikuwa Yesu Kristo. Angelikuwa Mwokozi wa watu wote ulimwenguni. Malaika wengi zaidi walikuja. Waliimba, “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

Picha
Alt text

Wachungaji walienda kwa haraka kumtembelea mtoto Yesu. Walifurahi sana kumuona!

Picha
Alt text

Wachungaji waliwaeleza wengine kuhusu Yesu Kristo. Walitaka kila mtu asikie habari hiyo njema.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Ninaweza Kuimba kuhusu Yesu Kristo

Picha
alt text here

Kielelezo na Apryl Stott

Ninaweza kuimba nyimbo kuhusu Yesu ili kusherehekea kuzaliwa Kwake.