Miito ya Misheni
Ujumbe wa Urais wa Kwanza


“Ujumbe wa Urais wa Kwanza,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Ujumbe wa Urais wa Kwanza,” Hubiri Injili Yangu

Ujumbe wa Urais wa Kwanza

Mpendwa Mmisionari Mwenzangu:

Tunakupongeza juu ya hii fursa kuu uliyonayo ya kuwa mmisionari wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hakuna kazi ya kuvutia sana au muhimu kuliko kuikusanya Israeli.

Hubiri Injili Yangu imekusudiwa ikusaidie uwe uliyejiandaa vyema, uwe mmisionari aliyekomaa zaidi kiroho. Na pia imekusudiwa ikusaidie uwe mwalimu mwenye ufanisi zaidi. Tunakusihi ukitumie kila siku katika kujifunza kwako binafsi na pamoja na mmisionari mwenza wako. Pia tunakuhimiza ukitumie katika mikutano yenu ya baraza la wilaya na mikutano ya kanda. Soma maandiko yaliyorejelewa na ujifunze mafundisho na kanuni.

Tunakualika uinue hisia mpya ya kujitolea kumsaidia Baba yetu wa Mbinguni katika kazi Yake tukufu. Kila mmisionari ana wajibu muhimu katika kumsaidia Bwana katika kazi Yake ya “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).

Bwana atakubariki unapojitolea mwenyewe kwa unyenyekevu kumtumikia Yeye. Na upate shangwe kuu na furaha unapofanya kazi miongoni mwa watoto wa Baba wa Mbinguni.

Urais wa Kwanza