Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 4


Sehemu ya 4

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa baba yake Joseph Smith Mkubwa, huko Harmony, Pennsylvania, Februari 1829.

1–4, Utumishi wa kishujaa huwaokoa wahudumu wa Bwana; 5–6, Sifa ya uchamungu huwapasisha wao kwenye huduma; 7, Mambo ya Mungu ni lazima yatafutwe.

1 Sasa tazama, kazi ya ajabu karibu yaja miongoni mwa wanadamu.

2 Hivyo basi, ninyi nyote ambao mnaingia katika utumishi wa Mungu, angalieni kwamba mnamtumikia yeye kwa moyo wenu wote, uwezo, akili na nguvu zenu zote, kwamba muweze kusimama pasipo lawama mbele za Mungu siku ile ya mwisho.

3 Kwa hivyo, kama unayo tamaa ya kumtumikia Mungu wewe umeitwa kwenye kazi hiyo;

4 Kwani tazama shamba ni jeupe tayari kwa mavuno; na lo, yeye aingizaye mundu yake kwa nguvu, ndiye huyo huyo ajiwekeaye ghalani akiba ili asiangamie, bali ajiletee wokovu kwa nafsi yake;

5 Na imani, tumaini, hisani na upendo, na jicho lake likiwa kwenye utukufu wa Mungu pekee, humpasisha mtu huyo katika kazi.

6 Kumbuka imani, wema, maarifa, kiasi, uvumilivu, upendano wa kindugu, uchamungu, hisani, unyenyekevu, jitihada.

7 Omba, nawe utapata; bisha, nawe utafunguliwa. Amina.