Misaada ya Kujifunza
TJS, Marko 14


TJS, Marko 14:20–26. Linganisha na Marko 14:22–25

Yesu anaanzisha sakramenti kamaukumbusho wa mwili na damu Yake.

20 Na wakiwa wanakula, Yesu alitwaa mkate na akaubariki, akaumega, na akawapa, akisema, Twaeni, na mle.

21 Tazama, hii ni kwa ajili yenu kufanya katika ukumbusho wa mwili wangu; maana kila wakati mfanyapo hivi mtaikumbuka saa hii ambayo nilikuwa pamoja nanyi.

22 Na akatwaa kikombe, na alipomaliza kushukuru, akawapa wao; nao wote wakanywa.

23 Naye akawaambia, Hii ni katika ukumbusho wa damu yangu ambayo inamwagika kwa ajili ya wengi, na kwa agano jipya ambalo ninalitoa kwenu; maana ninyi mtanishuhudia ulimwenguni kote.

24 Na kila wakati mfanyapo ibada hii, mtanikumbuka mimi katika saa hii ambayo nilikuwa pamoja nanyi na kunywa kikombe hiki, hata wakati wa mwisho wa huduma yangu.

25 Amini ninawaambia, Juu ya hili mtashuhudia; maana sitakunywa tena kabisa uzao wa mizabibu pamoja nanyi, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.

26 Na sasa walisikitishwa, na walimlilia.

TJS, Marko 14:36–38. Linganisha na Marko 14:32–34

Huko Gethsemani, hata baadhi ya Mitume Kumi na Wawili hawatambui kiukamilifu nafasi ya Yesu kama Masiya.

36 Na wakaja mahali palipoitwa Gethsemani, iliyokuwa bustani; na wanafunzi wake wakaanza kustajabia kupita kiasi, na kutatizwa, na kunungʼunika mioyoni mwao, wakijiuliza kama huyu ndiye Masiya.

37 Na Yesu akijua mioyo yao, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, muda niombapo.

38 Na akawatwaa pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana, na akawakemea, na akiwaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi, hata kiasi cha kufa; kaeni hapa na mkeshe.