Misaada ya Kujifunza
TJS, Marko 3


TJS, Marko 3:21–25. Linganisha na Marko 3:28–30

Yesu atawasamehe wenye dhambi wote wanaotubu isipokuwa wale wanaokufuru dhidi ya Roho Mtakatifu.

21 Na kisha wakamjia watu fulani, wakimshitaki, wakisema, Kwa nini unawapokea wenye dhambi, wakati unajifanya wewe ni Mwana wa Mungu.

22 Lakini aliwajibu na akasema, Amini nawaambia, Dhambi zote ambazo binadamu amezifanya, watakapo tubu, watasamehewa; kwani nimekuja kuhubiri toba kwa wana wa watu.

23 Na kufuru, kwa hii na kwa vyovyote vile watakao kufuru, watasamehewa wale ambao watakuja kwangu, na kufanya yale ambayo wanaona mimi nafanya.

24 Lakini kuna dhambi ambayo haitaweza kusamehewa. Yule ambaye atakufuru dhidi ya Roho Mtakatifu, kamwe hana msamaha; lakini yupo katika hatari ya kuteseka kifo cha kiroho. Na atarithi laana ya milele.

25 Na hii aliwaambia kwa sababu walisema, ana pepo mchafu.