Mkutano Mkuu
Utamaduni wa Kristo
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2020


Utamaduni wa Kristo

Tunaweza kufurahia tamaduni zetu nzuri za kidunia na kuwa washiriki kikamilifu katika utamaduni wa milele utokao kwenye injili ya Yesu Kristo.

Ni ulimwengu mkubwa ulioje sisi tunamoishi na kushirikiana na wengine, nyumbani kwa watu wenye utofauti mkubwa, lugha, mila, na historia—iliyo enea kwenye mamia ya nchi na maelfu ya makundi, kila moja likiwa tajiri katika utamaduni. Mwanadamu anavyo vingi vya kujivunia na kusherehekea. Lakini ingawa ni tabia ya kujifunza—vile vitu ambavyo tumeachiwa tuvione katika utamaduni ambamo ndani yake tunakua —unaweza kutupa nguvu kubwa katika maisha yetu, unaweza pia, kwa wakati fulani, kuja kuwa kikwazo kikubwa.

Inaweza kuonekana kwamba utamaduni umezama sana katika fikira zetu na kwamba tabia haiwezekani kubadilishwa. Na, hata hivyo, sehemu kubwa ya kile tunachohisi ndicho kinachotuelezea sisi na kutokana na hicho tunahisi ndio utambulisho wetu. Unaweza ukawa ndio nguvu kubwa kiasi kwamba tukashindwa kuona udhaifu wa kutengenezwa na binadamu au ni dosari katika utamaduni wetu sisi wenyewe, matokeo yake ni kutotaka kutupilia mbali baadhi ya “desturi za mababu zetu.” Kutawaliwa kupita kiasi na utambulisho wa kiutamaduni kunaweza kumwongoza mtu kukataa mawazo, sifa, na desturi—za kustahili—hata kumchamungu.

Nilimjua mwanamume muungwana wa kupendeza, siyo miaka mingi iliyopita, ambaye anasaidia kueleza kwa mifano kanuni hii ya kiulimwengu ya utamaduni wa kutoweza kuona mbali. Kwanza nilionana naye huko Singapore wakati nilipopangiwa kuwa mwalimu wa nyumbani wa familia yake. Profesa maarufu wa Sankrit na Tamil, yeye alitokea kusini mwa India. Mke wake mpendwa na wana wawili walikuwa ni waumini wa Kanisa, lakini yeye hakuwa amejiunga na Kanisa wala kusikiliza sana kuhusu mafundisho ya injili. Alikuwa akifurahia jinsi mke wake na wanawe walivyokuwa wakiendelea na aliwasaidia kikamilifu katika shughuli zao na wajibu wao kwa Kanisa.

Wakati nilipomwomba kumfundisha kanuni za injili na kushirikiana naye imani yetu, mwanzoni alisita. Ilinichukua muda kugundua kwa nini: alijisikia kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa msaliti wa uzamani wake, watu wake, na historia yake! Kulingana na njia zake za kufikiri, yeye angekuwa anakataa kila kitu cha yeye alichokuwa, kila kitu familia yake ilichomfundisha awe, urithi wake halisi wa Kihindi. Kwa miezi michache iliyofuata, tulikuwa tumeweza kuongelea kuhusu mambo haya. Niliingiwa na hofu (ingawa sikushangaa) kwa jinsi injili ya Yesu Kristo ilivyoweza kumfungua macho yake ili kuona mambo tofauti.

Katika tamaduni nyingi za kutengenezwa na mwanadamu kumepatikana vyote mema na mabaya, yenye kujenga na yenye kuangamiza.

Matatizo yetu mengi ya kidunia ni matokeo ya moja kwa moja ya migongano baina ya yale mawazo na desturi zinazochomoza kutoka kwenye utamaduni wao. Lakini kwa kweli lakini sio bayana migogoro na machafuko yote kwa haraka ingefifia kama tu ulimwengu ungekubali “Utamaduni wa Asili,” ambao sote tuliumiliki sio miaka mingi iliyopita. Utamaduni huu unarudi nyuma hadi kwenye maisha yetu kabla ya kuzaliwa. Ulikuwa utamaduni wa Adamu na Henoko. Ulikuwa ni utamaduni ulianzishwa juu ya msingi wa mafundisho ya Mwokozi katika Wakati wa Meridiani, na unapatikana tena kwa wanawake wote na wanaume katika siku yetu. Ni wa kipekee. Ndiyo “mkuu kushinda wote” na unakuja kutoka katika mpango mkuu wa furaha, uliasisiwa na Mungu na Kuletewa ushindi na Kristo. Unaunganisha zaidi kuliko kugawa. Unaponya zaidi kuliko kudhuru.

Injili ya Yesu Kristo inatufundisha sisi kwamba kuna lengo katika maisha.hunialika. Kuwepo kwetu hapa siyo ajali moja kubwa ya ulimwengu au kimakosa! Tuko hapa kwa sababu.

Utamaduni huu msingi wake ni ushuhuda kwamba Baba yetu wa Mbinguni yu hai, kwamba ni halisi, na anampenda kila mmoja wetu, binafsi. Sisi ni “kazi [Yake] na utukufu [Wake].” 1 Inaoana na dhana ya usawa wa ustahili. Hakuna utambulisho wa tabaka au daraja. Sisi, hata hivyo, ni kaka na kaka, watoto halisi wa kiroho wa—Wazazi wa Mbinguni. Hakuna kubagua au “sisi dhidi ya wao” kifikira katika ule “utamaduni mkuu wa tamaduni zote. Sote ni “sisi.” Sote ni “wao.”. Tunaamini kwamba tunawajibu na kuwajibika kwa ajili yetu wenyewe, kila mmoja, Kanisa, na ulimwengu wetu. Wajibu na kuwajibika ni vipengele muhimu katika makuzi yetu.

Hisani, kujali kweli kama Kristo, ndio kiini cha utamaduni huu. Tunajisikia masikitiko ya kweli kwa shida za mwanadamu mwenzetu, kimwili na kiroho, na kufanyia kazi masikitiko hayo. Hii inafukuza kubagua na chuki.

Tunafurahia utamaduni wa ufunuo, kitovu chake ni neno la Mungu kama linavyopokelewa na manabii (na kuthibitishwa kibinafsi kwa kila mmoja wetu kupitia kwa Roho Mtakatifu). Wanadamu wote wanaweza kujua mapenzi na mawazo ya Mungu.

Utamaduni huu unalinda kanuni ya haki ya kujiamulia. Uwezo wa kuchagua ni muhimu zaidi kwa maendeleo yetu na furaha yetu. Kuchagua kwa busara ni muhimu zaidi.

Ni utamaduni wa kusoma na kujifunza. Tunatafuta maarifa na hekima na vilivyo bora katika vitu vyote.

Ni utamaduni wa imani na utii. Imani katika Yesu Kristo ni kanuni ya kwanza ya utamaduni wetu na utiifu kwa mafundisho na amri zake ni matokeo. Haya yanatoa kuinuka kwa uwezo wa kujitawala.

Ni utamaduni wa maombi. Tunaamini kwamba Mungu sio tu atatusikia, bali pia atatusaidia.

Ni utamaduni wa maagano na ibada, maadili ya viwango vya juu, kutoa dhabihu, msamaha na toba, na kujali hekalu la miili yetu. Hivi vyote ni ushahidi wa msimamo wetu kwa Mungu.

Ni utamaduni unaotawaliwa na ukuhani, mamlaka ya kutenda katika jina la Mungu, nguvu ya Mungu ya kuwabariki watoto Wake. Inawajenga na kuwawezesha watu binafsi kuwa watu bora zaidi, viongozi, akina mama, akina baba na wenzi—na unaitakasa nyumba.

Miujiza mingi ya kweli inapatikana katika huu, wa kale zaidi ya tamaduni zote, ilifanyika kwa imani katika Yesu Kristo, nguvu ya ukuhani, maombi, maboresho binafsi, uongofu wa kweli, na msamaha.

Ni utamaduni wa kazi ya umisionari. Thamani ya nafsi ni kuu.

Katika utamaduni wa Kristo, wanawake wanapandishwa kwenye hadhi yao sahihi na ya milele. Wao sio watumishi wasaidizi kwa wanaume, kama kwenye tamaduni nyingi katika ulimwengu wa leo, lakini ni wakamilifu na wabia walio sawa hapa na katika ulimwengu ujao.

Utamaduni huu unaunga mkono utakatifu wa familia Familia ni kitengo cha msingi cha umilele. Ukamilifu wa familia unastahili dhabihu yo yote kwa sababu, kama ilivyofundishwa, “hakuna mafanikio mengine yo yote yanayoweza kufidia kushindwa katika nyumba.” 2 Nyumbani ndiyo mahali kazi bora zaidi inafanyika na ndipo furaha yetu kuu zaidi inapopatikana.

Katika utamaduni wa Kristo kuna mtazamo—na fokasi na mwelekeo wa milele. Utamaduni huu unajali mambo yenye thamani ya kudumu! Inakuja kutoka katika injili ya Yesu Kristo, ambayo ni ya milele, inaelezea zile “kwa nini,” “nini” na “wapi” juu ya kuwepo kwetu. (Ina jumuisha , na haitengi.) Kwa sababu utamaduni huu unatokana na matumizi ya mafundisho ya Mwokozi inasaidia kutoa mkono wa uponyaji ambao ulimwengu wetu unauhitaji sana.

Ni baraka iliyoje kuwa sehemu ya njia hii kuu na maarufu ya maisha! Kuwa sehemu ya huu, utamaduni Mkuu wa Tamaduni zote, kunahitajika mabadiliko. Manabii wamefundisha kwambani muhimu kuacha nyuma kitu cho chote katika tamaduni zetu za zamani ambazo haziendani na Utamaduni wa Kristo. Lakini hii haimaanisha kwamba tunapaswa kuacha nyuma kila kitu. Manabii pia wamesisitiza kwamba tunaalikwa, mmoja na wote, kuleta imani yetu na vipaji vyetu na maarifa—vyote ambavyo ni vizuri katika maisha yetu na tamaduni zetu—pamoja na sisi, na tuache Kanisa “liongezee” kupitia ujumbe wa injili. 3

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho si jumuiya ya kimagharibi au kitu cha utamaduni wa Kimarekani. Na ni Kanisa la Kimataifa, kama ilivyokuwa daima iwe. Zaidi ya hivyo, ni la kutoka mbinguni Waumini wapya kutoka kote ulimwenguni wanaleta utajiri, utofauti, na msisimko ndani ya familia inayokua daima. Watakatifu wa Siku za Mwisho kila mahali bado wanasherehekea na kuheshimu urithi na mashujaa wao wenyewe, lakini sasa wao pia ni sehemu ya kitu fulani kikubwa zaidi. Utamaduni wa Kristo unatusaidia kujiona sisi wenyewe kama kweli tulivyo, na tukisha jiona kupitia lensi za milele, zilizo punguzwa nguvu na haki, hutumika kuongeza uwezo wetu wa kutimiza mpangocmkuu wa furaha.

Hivyo, nini kilitokea kwa rafiki yangu? Vyema, alifundishwa masomo na akajiunga na Kanisa. Familia yake tangu hapo imefungwa kwa muda na milele yote katika Hekalu huko Sidney. Yeye ameacha machache—na amepata kila kitu. Alikuja kugundua kwamba anaweza bado kusherehekea historia yake, na bado akajivunia jadi yake. Amejionea kwamba hakuna matatizo kushirikisha utamaduni wa eneo lake husika katika Mkuu wa Tamaduni zote. Aligundua kwamba kuleta hiyo ambayo inalingana na ukweli na haki kutoka maisha yake ya zamani ndani ya utamaduni wake mpya inatumika kuboresha tu ushirika wake na Watakatifu na kusaidia kuwaunganisha wote kama wamoja katika Jumuiya ya Mbinguni.

Tunaweza, ndiyo, sote kufurahia yaliyo bora zaidi katika tamaduni zetu za kidunia za kila mtu na bado tukawa washiriki kamili katika utamaduni mkongwe wa tamaduni zote- wa mwanzo, wa mwisho utamaduni wa milele ambao unakuja kutokana na injili ya Yesu Kristo. Ni urithi mzuri ulioje ambao sote tunashirikiana. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Musa 1:39.

  2. Mafundisho ya Marais wa Kanisa: David O. McKay (2011), 154.

  3. Ona Teachings of Presidents of the Church: George Albert Smith (2011), xxviii; Gordon B. Hinckley, “The Marvelous Foundation of Our Faith,” Liahona, Nov. 2002, 78–81.