2010–2019
Usitazame Karibu, Tazama Juu!
Aprili 2017


Usitazame Karibu, Tazama Juu!

Kuwaalika wengine kuja kwa Kristo ni lengo letu, na tunaweza kutimiza lengo hili kwa kutazama juu kwa Yesu Kristo.

Lengo langu ni “kuwaalika wengine kuja kwa Kristo.”1 Hili ni lengo lako pia. Tunaweza kamilisha lengo hili kwa kutazama juu kwa Yesu Kristo.

Picha
Familia ya Mzee Choi

Nilibatizwa pamoja na wazazi wangu nilipokuwa na umri wa miaka 16. Mdogo wangu, Kyung-Hwan, aliyekuwa na umri wa miaka 14, alijiunga na kanisa kupitia mjomba wangu, Young Jik Lee, na akatualika katika kanisa lake. Kila mtu kati ya watu 10 katika familia yetu alikuwa katika kanisa tofauti, hivyo tulifurahi kuupata ukweli na tulitaka kushiriki furaha ile tuliyopata katika injili ya Yesu Kristo baada ya kubatizwa.

Picha
Baba ya Mzee Choi na wengine

Baba yangu alikuwa na hamasa kuliko wote kujifunza na kushiriki ukweli. Alikuwa akiamka mapema asubuhi kujifunza maandiko kwa masaa mawili kila siku. Baada ya kazi alienda na wamisionari kutembelea familia, marafiki na majirani karibu kila siku. Miezi saba baada ya kubatizwa kwetu, watu 23 wa familia yangu pamoja na jamaa yangu walikuwa waumini wa kanisa. Hilo lilifuatiwa na muujiza wa kuona watu 130 wakibatizwa mwaka uliofuata kupitia kazi ya muumini mmisionari ya Baba yangu.

Picha
Mwanzoni wa kazi ya umisionari
Picha
Kazi ya umisionari iliyopanuliwa

Historia ya familia ilikuwa ni muhimu pia kwake, na alimaliza vizazi nane vya mababu zetu. Tangu wakati ule na kuendelea, matunda ya kuongoka kwa familia yetu, yalianza na kaka yangu mwenye miaka 14, yameongezeka katika njia zisizohesabika sio tu kwa wanaoishi lakini pia kwa wafu. Tukijenga juu ya kazi ya baba yangu na wengine, mti wa familia yetu sasa umekua hadi vizazi 32, na sasa tunamalizia kazi ya hekalu katika matawi mengi. Leo ninashangaa na kuhisi shangwe kuu ikituunganisha na mababu na wajukuu.

Picha
Historia ya familia iliyopanuliwa

Rais Gordon B. Hinckley alinakili uzoefu kama huu katika Hekalu la Columbus Ohio.

“Nikitazama katika maisha ya [baba ya babu yangu, babu yangu, na Baba] wakati nilikaa Hekaluni, nilimtazama binti yangu, na binti mkujuu, … na kwa watoto wake, vitukuu. Ghafla nilitambua kuwa nilisimama katikati ya vizazi saba—vitatu kabla yangu na vitatu baada yangu.

“Katika nyumba ile takatifu na iliyotakaswa ilipita katika akili yangu hisia ya jukumu kubwa lililokuwa langu ambalo ninapaswa kurithisha vyote nilivyopata kutoka kwa babu zangu kwa vizazi vilivyokuja baada yangu.”2

Picha
Katikati ya vizazi vyetu

Sisi wote tupo katikati ya familia ya milele. Jukumu letu linaweza kuwa hatua ya kugeuka ambapo mabadiliko muhimu yanaweza kutokea katika njia hasi au chanya. Rais Hinckley aliendelea, “Kamwe usikukali wewe binafsi kuwa kiungo dhaifu katika mlolongo wa vizazi vyako.”3 Uaminifu wako katika injili utaimarisha familia yako. Ni kwa jinsi gani tunaweza hakikisha tutakuwa kiungo imara katika familia yetu ya milele?

Siku moja, miezi michache baada ya ubatizo wangu, nilisikia baadhi ya waumini wakikosoana katika kanisa. Nilifadhaika sana. Nilirudi nyumbani na kumwambia baba yangu kwamba labda nisiende kanisani tena. Ilikuwa vigumu kuona waumini wakikosoa wengine hivyo. Baada ya kusikiliza, baba yangu aliniambia kwamba injili ilirejeshwa na ni kamilifu lakini waumini bado, wala si yeye mwenyewe na hata mimi. Kwa uthabiti alisema, “usipoteze imani yako kwa sababu ya watu wanaokuzunguka, lakini jenga uhusiano imara na Yesu Kristo. Usitazame karibu, tazama juu!”

Tazamu juu kwa Yesu Kristo—ushauri wa hekima wa baba yangu, unaimarisha imani yangu kila ninapopata changamoto katika maisha. Alinifundisha jinsi ya kuishi mafundisho ya Yesu, tulipokuwa tukisoma maneno haya. “Nitumaini katika kila jambo, usihofu, usiogope.”4

Picha
Wamisonari katika Hekalu la Seattle Washington

Nilipokuwa nikiongoza katika misheni ya Washington Seattle, mvua ilinyesha katika siku nyingi za mwaka. Bado, wamisionari walielekezwa kuenda nje na kuhamasisha watu katika mvua. Nilikuwa nikiwaambia, “Nendeni nje katika mvua, tazameni juu mbinguni, fungueni midomo yenu, na mnywe! Ukitazama juu, utaimarishwa kuweza kufungua mdomo kwa kila mtu pasipo woga.” Ilikuwa ni somo la ishara kwao kutazama juu wakati wanapokumbwa na changamoto hata baada ya misheni. Tafadhali usijaribu hili katika maeneo machafu.

Wakati nikikuhudumu katika misheni ya Seattle, nilipokea simu kutoka kwa mtoto wangu mkubwa wa kiume, Sunbeam, ambaye ni mcheza kinanda. Alisema atakuwa na bahati ya kucheza katika ukumbi wa Carnegie huko New York kwa sababu alishinda shindano la kimataifa. Tulikuwa na furaha sana na kusisimka kwa ajili yake. Hata hivyo, jioni ile, wakati tunasali kwa shukurani, mke wangu alitambua hatungeweza ungana naye katika maonyesho na akasema kwa Baba wa Mbinguni kitu kama hiki: “Baba wa Mbinguni, ninashukuru kwa baraka ambazo umempatia Sunbeam. Hata hivyo, ninasikitika kuwa sitoweza enda huko. Ningeliweza endapo Ewe ungelitoa baraka hii walau kabla au baada ya misheni hii. Silalamiki, lakini ninahisia kidogo ya huzuni.”

Pindi tu alipomaliza sala hii, alisikia sauti dhahiri. “Kwa sababu huwezi enda, ndio maana mtoto wako amepewa hii bahati. Ungelipenda kubadilisha?”

Mke wangu alishangazwa. Alijua watoto wangelibarikiwa kupitia kazi ya uaminifu ya wazazi wao katika ufalme wa Bwana. Lakini ilikuwa mara ya kwanza alifahamu jukumu lake kwa uwazi kama huo. Alimjibu mara moja. “Hapana, hapana, ni SAWA kwangu mimi kutoenda. Acha yeye apate hiyo heshima.”

Kaka na dada zangu wapendwa, si rahisi kwetu kutambua upendo wa Baba wa Mbinguni wakati tunatazama karibu kwa macho yetu ya kimwili kwa sababu tunaona maudhi, hasara, mizigo, au kwanza upweke. Kwa upande mwingine, tunaweza ona baraka nyingi zaidi tunapotazama juu. Na kama tunapata baraka yoyote kutoka kwa Mungu, ni kutokana na utii kwa sheria ile ambayo juu yake hutoka.5 Kwa wale wote ambao wameingia katika huduma yoyote ya Mungu, jueni kwamba ninyi ni kiunganishi imara cha baraka kuu kwa wale waliowatangulia na vizazi baada yenu.

Leo, ninashukuru kuona wana familia wetu wengi ni waaminifu katika maagano na nahuzunishwa kuona viti vilivyo wazi jirani yetu. Mzee M. Russell Ballard alisema: “Kama utachagua kulegea au kuacha Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho la urejesho, utaenda wapi? Utafanya nini? Uamuzi wa “kutotembea tena” na waumini wa Kanisa na viongozi wateule wa Bwana utakuwa na athari ya muda mrefu ambayo haiwezi kuonekana hivi sasa.6 Rais Thomas S. Monson alituhamasisha, “Na tuchague siku zote usahihi mgumu kuliko urahisi potofu,”7

Wakati haujapita kumtengemea Yesu Kristo. Mikono Yake daima ipo wazi kwako. Kuna vizazi kabla yetu na baada yetu vinatutegemea sisi kumfuata Kristo ili tuweze kuwa familia ya milele ya Mungu.

Nilipopumzishwa katika mwito wangu kama rais wa kigingi, watoto wangu wa kiume walisisimka kwamba wangekuwa na muda mwingi nami. Wiki tatu baadae niliitwa kama Sabini. Mwanzoni nilidhani wangekuwa wamefadhaishwa, lakini jibu nyenyekevu la mtoto wangu mdogo kabisa wa kiume lilikuwa, “Baba, usijali. Sisi ni familia ya milele.” Ni ukweli gani mfupi na bayana ulikuwa! Nilikuwa na wasiwasi kidogo kwa sababu nilitazama karibu katika maisha haya ya duniani tu, lakini mtoto wangu alifurahi kwa sababu hakutazama hapa lakini alitazama juu na macho yake kuelekea umilele na malengo ya Bwana.

Si rahisi wakati wote kutazama juu pindi wazazi wako wanapinga injili, pindi wewe ni muumini wa tawi dogo la kanisa, pindi mwenza wako si muumini, pindi wewe bado hujaoa ingawa umefanya juhudi kuoa, pindi mtoto amepotoka, pindi wewe ni mzazi pekee, pindi una matatizo kimwili au kimhemko, au pindi wewe ni mwadhiriwa katika janga, na kadhalika. Shikilia imani yako katika nyakati hizo ngumu. Tazama juu kwa Kristo kwa nguvu, uwiano, na uponyaji. Kupitia nguvu ya upatanisho wa Yesu Kristo, “vitu vyote vitafanyakazi kwa manufaa yako.”8

Natoa ushahidi wa Yesu Kristo, kwamba Yeye ni Mwokozi na Mkombozi. Tukimfuata nabii wetu anayeishi, Rais Thomas S. Monson, tunakuwa tunatazama juu kwa Yesu Kristo. Tunaposali na kujifunza maandiko kila siku, na kushiriki kwa dhati katika sakramenti kila wiki, tunapata kumtazama Yeye daima . Ninafuraha kuwa muumini wa kanisa hili na kuwa sehemu ya familia ya milele. Napenda kushiriki injili hii kuu na watu wengine. Kuwaalika wengine kuja kwa Kristo ni lengo letu, na tunaweza kutimiza lengo hili kwa kutazama juu kwa Yesu Kristo. Kwa unyenyekevu nashuhudia vitu hivi katika jina la Yesu Kristo, amina.