2010–2019
Twende kwa Nani?
Oktoba 2016


Twende kwa Nani?

Mwishowe, kila mmoja wetu lazima ajibu swali la Mwokozi: “Je, Ninyi nanyi mwataka kuondoka?

Miaka kadhaa iliyopita, familia yangu na mimi tulitembelea Nchi Takatifu. Mojawapo ya kumbukumbu yangu kutoka kwenye safari ilikuwa ni kutembelea chumba cha juu katika Yerusalemu, sehemu ya jadi ya Pasaka.

Niliposimama katika eneo lile, nilisoma kutoka Yohana 17, sehemu ambayo Yesu alimwomba Baba Yake kwa ajili ya wafuasi Wake:

“Ninawaombea wao … ili wawe wamoja, kama sisi tulivyo. …

“Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao;

“Naomba ili wote wawe kitu kimoja; kama wewe, Baba, kama vile wewe ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, ili nao waweze kuwa kitu kimoja na sisi.”1

Niliguswa moyo sana nilipokuwa ninasoma maneno haya na nikajikuta naomba katika sehemu ile takatifu ili mimi niweze kuwa pamoja na familia yangu na pamoja na Baba yangu wa Mbinguni na pamoja Mwanawe.

Uhusiano wetu wa thamani na familia, marafiki, Bwana, na Kanisa Lake lililorejeshwa ni miongoni mwa vitu ambavyo ni muhimu katika maisha. Kwa sababu mahusiano haya ni muhimu sana, yanatakiwa yatunzwe, yalindwe, na yastawishwe.

Moja ya hadithi inayoumiza moyo katika maandiko ilitokea wakati “wengi wa wafuasi wa [Bwana]” waliona ni vigumu kukubali mafundisho Yake, na “wakarudi nyuma, na hawakutembea tena pamoja naye.2

Wakati wafuasi hawa walipoondoka, Yesu akawageukia Kumi na Wawili na kuwauliza, “Nanyi pia mwataka kwenda zenu?”3

Petro akajibu:

“Bwana, twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

“Na sisi tunaamini na tunajua kwamba wewe ndiye yule Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”4

Kwa wakati ule, wakati wengine wakilenga mambo ambayo wasingeyakubali, Mitume walichagua kulenga yale waliyoyaamini na kuyajua, na kwa hivyo, walibaki na Kristo.

Baadaye, siku ya Pentekosti, Wale Kumi na Wawili walipokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Wakasimama imara katika ushuhuda wao wa Yesu na wakaanza kuelewa zaidi mafundisho ya Yesu.

Leo hakuna tofauti. Kwa wengine, mwaliko wa Kristo wa kuamini na kubaki unaendelea kuwa mgumu—au vigumu kuukubali. Wanafunzi wengine wanapata shida kuelewa sera mahususi za Kanisa au mafundisho. Wengine hupata wasiwasi katika historia yetu au katika udhaifu wa baadhi ya waumini na viongozi, wa zamani na sasa. Bado wengine wanaona vigumu kuishi dini ambayo inahitaji zaidi. Mwisho, wengine “wanaogopa kufanya mema.”5 Kwa sababu hizi na zingine, baadhi ya waumini wa Kanisa hutangatanga katika imani zao, wakishangaa kama wanapaswa kuwafuata wale “walirudi nyuma, wasiandamane tena” na Yesu.

Kama kuna mmoja wenu anayegugumia katika imani yake, ninamuuliza swali kama alilouliza Petro: “Mtakwenda kwa nani [ninyi]?” Kama unachagua kuliacha Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho la urejesho, utakwenda wapi? Utafanya nini? Uamuzi wa “kutotembea tena” na waumini wa Kanisa na viongozi waliochaguliwa na Bwana utakuwa na athari ya muda mrefu ambayo haiwezi kuonekana hivi sasa. Kunaweza kuwa na mafundisho, baadhi ya sera, zikiwa na historia ambayo itakuweka pabaya na imani yako, na unaweza kuhisi kwamba njia pekee ya kutatua tatizo hili sasa ni “kutotembea tena” pamoja na Watakatifu Lakini kama utaishi muda mrefu kama mimi, utakuja kujua kwamba vitu vina njia ya kujitatua vyenyewe. Msukumo wa utambuzi au ufunuo unaweza kutoa mwanga mpya juu ya swala hilo. Kumbuka, Urejesho siyo tukio, bali unaendelea kutolewa.

Usiuache ukweli uliofunuliwa kupitia Nabii Joseph Smith. Usiache kusoma, kutafakari, na kutumia mafundisho ya Kristo yaliyomo kwenye Kitabu cha Mormoni.

Usiache kutoa muda sawa kwa Bwana kupitia jaribio la uaminifu ili kuelewa kile alichofunua Bwana. Kama rafiki yangu mpendwa na mwenzangu wa zamani Mzee Neal A. Maxwell aliwahi kusema, “Hatufai kufikiria … kwamba kwa sababu tu kitu hakielekezeki nasi, hakiwezi kuelezeka.”6

Hivyo kabla hujafanya uchaguzi huo wa kuondoka, ninakushauri acha na fikiria kwa makini kabla ya kukiacha kile kilichokuleta kwenye ushuhuda wako wa Kanisa la Yesu Kristo la urejesho hapo mwanzoni. Sita na ufikirie kuhusu ulivyojisikia hapa na kwa nini ulisikia hivyo. Fikiria kuhusu wakati ambao Roho Mtakatifu ametoa ushahidi kwako wa ukweli wa milele.

Utakwenda wapi kuwatafuta wengine wenye kuamini kama wewe, Wazazi wapendwa wa Mbinguni, wanaotufundisha kurudi kwenye makao yao ya milele?

Wapi utakwenda kufundishwa kuhusu Mwokozi ambaye ni rafiki yako mkubwa, ambaye hakuteseka tu kwa ajili ya dhambi zako bali pia aliteseka “maumivu na masumbuko na majaribio ya kila aina” hivyo “ ili kombe lake liweze kujaa neema, kutokana na mwili, kwamba aweze kujua kulingana na mapungufu ya mwili,”7 ikijumuisha, mimi ninaamini, udhaifu wa kukosa imani?

Wapi utakwenda kujifunza zaidi kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya furaha na amani ya milele, mpango ambao umejaa matarajio, mafundisho, na mwongozo mzuri kwa ajili ya maisha ya mwili na ya milele? Kumbuka, mpango wa wokovu unatoa maana ya maisha, malengo, na mwelekeo.

Ni wapi utakwenda kupata muundo wa Kanisa ambao ni wa kina ambao katika huo unafundishwa na kuungwa mkono na wanaume na wanawake ambao wana nia ya kumtumikia Bwana na kukuhudumia wewe na familia yako?

Ni wapi utakwenda kuwakuta manabii na mitume walio hai, ambao wameitwa na Mungu ili kukupa wewe nyenzo nyingine ya ushauri, kuelewa, kufariji, na kuhuishwa kwa ajili ya changamoto za leo?

Ni wapi utakwenda kuona watu wanaishi kulingana na maadili na misingi iliyowekwa ambao mnashiriki na kutaka kuwaachia watoto na wajukuu wako?

Na wapi utakwenda kupata furaha inayotokana na ibada za kuokoa na maagano ya hekalu?

Akina kaka na dada, kukubali na kuishi injili ya Kristo yaweza kuwa changamoto. Imekuwa hivyo kila mara, na itaendelea hivyo. Maisha yaweza kuwa kama watembeaji wakipanda mwinuko na ngazi ngumu. Ni jambo la asili na jambo la kawaida mara kwa mara kutulia katika njia ili kupata pumzi yetu, kuhesabu mizigo yetu, na kufikiria upya kasi yetu. Siyo kila mtu anahitaji kutulia katika njia, lakini hakuna kibaya kwa kufanya hivyo wakati mazingira yanaruhusu. Kwa kweli, inaweza kuwa kitu chanya kwa wale ambao huchukua nafasi kamili ya fursa ya kupata mahitaji wenyewe na maji ya hai wa Injili ya Kristo.

Hatari inakuja wakati mtu anapochagua kutangatanga kutoka kwenye njia iendayo kwenye mti wa uzima.8 Wakati mwingine tunaweza kujifunza na kutafiti na kujua, na wakati mwingine tunatakiwa kuamini, na kutumaini.

Mwishowe, kila mmoja wetu lazima ajibu swali la Mwokozi: “Je, Ninyi nanyi mwataka kuondoka?9 Sisi wote tunatakiwa kutafuta majibu yetu wenyewe kwa swali hilo. Kwa wengine, jibu ni rahisi, kwa wengine, ni gumu. Sijifanyi kujua kwa nini imani ya kuamini inakuwa rahisi kwa wengine kuliko wengine. Nina furaha kujua kwamba majibu yapo kila mara, na kama tunayatafuta—na kama kweli tunayatafuta kwa dhamira ya kweli na kwa lengo kamili la maombi ya moyo—sisi hatimaye tutapata majibu ya maswali yetu kama tutaendelea katika njia ya Injili. Katika kazi yangu ya uchungaji, nimejua wengi ambao walichepuka na kurudi baada ya jaribio la imani yao.

Matumaini yangu ya moyo ni kwamba tutapata na kualika idadi kubwa ya watoto wa Mungu ili kupata na kukaa kwenye njia ya injili ili wao pia “wale tunda, ambalo [ni] zuri kuliko matunda mengine yote.”10

Ombi langu la dhati ni kwamba sisi huwahamasisha, huwakubali, huwaelewa, na kuwapenda wale ambao wanasumbuka na imani zao. Hatutakiwi kamwe kuwatelekeza kaka na dada zetu. Wote tupo katika sehemu tofauti za njia, na tunahitaji kuhudumiana sisi kwa sisi ifaavyo.

Jinsi tunavyofungua mikono yetu katika roho ya kukaribisha waongofu wapya, pia lazima tukumbatie na kuwaunga mkono wale wenye maswali na wanaosumbuka na imani zao.

Kutumia mfano mwingine wa utambuzi, naomba mtu yeyote anayefikiria kuondoka “Meli ya Sayuni ya Kale,” ambapo Mungu na Kristo ni viongozi, watatulia na kufikiria kwa makini kabla ya kuondoka.

Tafadhali jua kwamba kupitia dhoruba kubwa ya upepo na mawimbi yaipigayo meli ya kale, Mwokozi yupo ndani na ana uwezo wa kukataza dhoruba kwa amri Yake, “Amani, itawale.” Hadi hapo, hatutakiwi kuogopa, na lazima tuwe na imani thabiti na kujua kwamba “hata upepo na mawimbi yanamtii.”11

Akina kaka na dada, ninawaahidi katika jina la Bwana kwamba Yeye hataliacha Kanisa Lake na kwamba Yeye hatamwacha yeyote kati yetu. Kumbuka jibu la Petro kwa swali na maneno ya Mwokozi:

“Twende kwa nani? wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

“Na sisi tunaamini na tunajua kwamba wewe ndiye yule Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”12

Ninashuhudia kwamba “hakuna jina lingine litatolewa wala njia ingine wala mbinu yoyote ambayo wokovu utawashukia watoto wa watu, ila katika na kupitia jina la Kristo.”13

Pia ninashuhudia kwamba Yesu Kristo amewaita mitume na manabii katika siku zetu na amerejesha Kanisa Lake pamoja na mafundisho na amri kama “kimbilio kutoka kwa dhoruba, na ghadhabu” ambayo hakika itakuja isipokuwa watu wa ulimwengu watubu na kumrudia Yeye.14

Ninashuhudia zaidi kwamba Bwana “anawakaribisha wote kuja kwake na kupokea wema wake; na hamkatazi yeyote anayemjia, wafungwa na waliohuru, wake kwa waume; … na wote ni sawa kwa Mungu.”15

Yesu ni Mwokozi na Mkombozi wetu, na injili Yake iliyorejeshwa itatuongoza salama kurudi katika uwepo wa Wazazi wetu wa Mbinguni kama tutabaki kwenye njia ya injili katika kufuata nyayo Zake. Juu yake mimi nashuhudia katika jina la Yesu Kristo, amina.