Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 130


Sehemu ya 130

Orodha ya mafundisho yaliyotolewa na Joseph Smith Nabii, huko Ramus, Illinois, 2 Aprili 1843.

1–3, Baba na Mwana wao wenyewe wanaweza kujionyesha kwa mwanadamu; 4–7, Malaika huishi katika mazingira ya selestia; 8–9, Dunia ya kiselestia itakuwa Urimu na Thumimu iliyo kuu; 10–11, Jiwe jeupe linatolewa kwa wote waingiao kwenye ulimwengu wa selestia; 12–17, Wakati wa Ujio wa Pili Nabii amefichwa; 18–19, Akili ipatikanayo katika maisha haya itafufuka pamoja nasi katika Ufufuko; 20–21, Baraka zote huja kwa kutii sheria; 22–23, Baba na Mwana wana miili ya nyama na mifupa.

1 Wakati Mwokozi aatakapojidhihirisha tutamwona kama alivyo. Tutamwona kuwa yeye ni bmtu kama sisi wenyewe.

2 Na kwamba uhusiano huu huu uliopo miongoni mwetu hapa utakuwepo miongoni mwetu kule, isipokuwa utazidishiwa autukufu wa milele, utukufu ambao sasa hatuufaidi.

3 Yohana 14:23—Kuonekana kwa aBaba na bMwana, katika mstari ule, ni ckujidhihirisha binafsi; na wazo la kwamba Baba na Mwana dwatakaa katika moyo wa mwanadamu ni wazo la zamani la kimadhehebu, na ni uongo.

4 Kama jibu kwa swali—Je, si kweli kwamba jinsi wakati aunavyopimwa kwa Mungu, kwa malaika, kwa manabii, na kwa wanadamu, hutegemea na sayari ambayo wao huishi?

5 Najibu, Ndiyo. Lakini hakuna amalaika ambao huhudumia dunia hii ila wale ambao ni wa dunia hii, au walikuwa wa dunia hii.

6 Malaika hawaishi katika sayari kama hii dunia;

7 Bali huishi mbele za Mungu, kwenye tufe mfano wa abahari ya kioo na bmoto, mahali ambapo mambo yote kwa ajili ya utukufu wao huonekana, yaliyopita, yaliyopo, na yajayo, na daima yapo mbele za Bwana.

8 Mahali ambapo Mungu hukaa ni aUrimu na Thumimu iliyo kuu.

9 aDunia hii, katika hali yake ya kutakaswa na isiyokufa, itafanywa kuwa mfano wa jiwe angavu kama kioo nayo itakuwa Urimu na Thumimu kwa wakazi wakaao juu yake, humo mambo yote yahusuyo ufalme mdogo, au falme zote za daraja la chini, zitaonekana kwa wale wakaao juu yake; na dunia hii itakuwa ya Kristo.

10 Ndipo jiwe jeupe lililotajwa katika Ufunuo 2:17, litakapokuwa Urimu na Thumimu kwa kila mmoja aliyepokea moja, ambalo kwalo hilo mambo yote yahusuyo falme za daraja la juu zitajulikana;

11 Na ajiwe jeupe limetolewa kwa kila mmoja wa wale wanaokuja katika ufalme wa selestia, ambapo juu yake bjina jipya limeandikwa, ambalo hakuna mtu ajuaye isipokuwa yeye yule mwenye kulipokea. Jina hilo jipya ni neno la ufunguo.

12 Ninatoa unabii, katika jina la Bwana Mungu, kwamba kuanza kwa amatatizo ambayo yatasababisha umwagaji mkubwa wa damu kabla ya kuja kwa Mwana wa Mtu yataanzia bCarolina ya Kusini.

13 Huenda ikaanza kutokana na swali la utumwa. Hii sauti iliniambia, wakati nilipokuwa nikiomba kwa dhati juu ya jambo hili, Desemba, 25, 1832.

14 Nilikuwa wakati mmoja nikiomba kwa dhati kujua wakati wa akuja kwa Mwana wa Mtu, wakati niliposikia sauti ikirudia yafuatayo:

15 Joseph, mwanangu, kama wewe utaishi mpaka kufikia umri wa miaka themanini na tano, utauona uso wa Mwana wa Mtu; kwa hiyo, acha hiyo yatosha, acha usinisumbue zaidi juu ya jambo hili.

16 Hivyo niliachwa, bila kuweza kuamua kama ujio huu unaozungumziwa ni kuanzia kwa milenia au ni baadhi ya kuonekana kwake kabla, au kama lazima nife na hivyo ndipo niuone uso wake.

17 Ninaamini ujio wa Mwana wa Mtu hautakuwa mapema kabla ya wakati huo.

18 Kanuni yoyote ya aakili tuipatayo katika maisha haya, itafufuka pamoja nasi katika bufufuko.

19 Na kama mtu anapata amaarifa na akili katika maisha haya kwa njia ya bjuhudi yake na cutii kuliko mwingine, yeye atakuwa na dheri ya juu zaidi katika ulimwengu ujao.

20 Kuna asheria, isiyotenguliwa iliyowekwa mbinguni bkabla ya misingi ya ulimwengu huu, ambapo juu yake cbaraka zote hutoka—

21 Na kama tunapata baraka yoyote kutoka kwa Mungu, ni kutokana na utii kwa sheria ile ambayo juu yake hutoka.

22 aBaba ana bmwili wa nyama na mifupa wenye kushikika kama wa mwanadamu; na Mwana vile vile; lakini cRoho Mtakatifu hana mwili wa nyama na mifupa, bali ni mtu wa Kiroho. Kama isingekuwa hivyo, Roho Mtakatifu asingeweza kukaa ndani yetu.

23 Mwanadamu aweza kumpokea aRoho Mtakatifu, na anaweza kushukia juu yake na asikae pamoja naye.