Misaada ya Kujifunza
Malaika


Malaika

Kuna aina mbili za viumbe katika mbingu vinavyoitwa malaika: wale ambao ni roho na wale wenye miili ya nyama na mifupa. Malaika walio roho tu bado hawajapata mwili wa nyama na mifupa, au ni roho wale ambao mwanzo walikuwa na miili ya kuharibika na sasa wanasubiri ufufuko. Malaika walio na miili ya nyama na mifupa ni kwamba ama wamekwisha kufufuka kutoka kwa wafu au wamehamishwa.

Kuna kumbukumbu nyingi katika maandiko ya kazi za malaika. Wakati mwingine malaika huongea kwa sauti ya radi kama wanatoa ujumbe wa Mungu (Mos. 27:11–16). Watu walio duniani wenye haki waweza pia kuitwa malaika (TJS, Mwa. 19:15 [Kiambatisho]). Baadhi ya malaika hutumikia kuzunguka kiti cha enzi cha Mungu mbinguni (Alma 36:22).

Maandiko pia huzungumzia juu ya malaika wa ibilisi. Hawa ni roho wale waliomfuata Lusiferi nao wakafukuzwa kutoka katika uwepo wa Mungu katika maisha kabla ya kuzaliwa na wakatupwa chini duniani (Ufu. 12:1–9; 2 Ne. 9:9, 16; M&M 29:36–37).