Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 19


Sehemu ya 19

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith, huko Manchester, New York, yawezekana kabisa ilikuwa katika kiangazi cha 1829. Katika historia yake, Nabii alitambulisha hii kama “amri ya Mungu na siyo ya mwanadamu, kwa Martin Harris, iliyotolewa na yeye aliye wa Milele.”

1–3, Kristo anao uwezo wote; 4–5, Watu wote lazima watubu au wateseke; 6–12, Adhabu ya milele ni adhabu ya Mungu; 13–20, Kristo aliteseka kwa ajili ya wote, kwamba wao wasiteseke kama watatubu; 21–28, Hubiri injili ya toba; 29–41, Tangaza habari njema.

1 Mimi ni aAlfa na Omega, bKristo Bwana; ndiyo, Mimi ndiye, mwanzo na mwisho, Mkombozi wa ulimwengu.

2 Mimi, nikiwa nimefanikisha na akutimiza mapenzi yake yeye niliye wake, hata Baba, juu yangu—nikiwa nimefanya hili ili niweze bkuvitiisha vitu vyote chini yangu—

3 Nikishikilia anguvu zote, hata ya bkumwangamiza Shetani na kazi zake hapo cmwisho wa dunia, na siku ile kuu ya hukumu, ambayo nitaipitisha juu ya wakazi wake, dnikimhukumu kila mtu kulingana na ekazi zake na matendo ambayo ameyafanya.

4 Na ni hakika kila mwanadamu ni lazima aatubu au bateseke, kwani Mimi, Mungu, sina cmwisho.

5 Kwa hiyo asijafuta hukumu ambayo nitaipitisha, lakini huzuni itajitokeza, kilio, bkuomboleza na kusaga meno, ndiyo, kwa wale ambao watapatikana katika mkono wangu wa ckushoto.

6 Hata hivyo, ahaikuandikwa kwamba hapatakuwa na mwisho wa mateso haya, bali imeandikwa bmateso yasiyo na mwisho.

7 Tena, imeandikwa alaana ya milele; kwa hiyo hii ni wazi zaidi kuliko maandiko mengine, ili liweze kufanya kazi katika mioyo ya wanadamu, kwa ajili ya utukufu wa jina langu.

8 Kwa hivyo, nitakuelezea wewe siri hii, kwani ni muhimu kwako kujua hata kama mitume wangu.

9 Ninasema kwenu ninyi ambao mmechaguliwa katika jambo hili, kama vile mmoja, ili kwamba muweze kuingia katika apumziko langu.

10 Kwani, tazama, asiri ya uchamungu, ni kuu namna gani! Kwani, tazama, Mimi sina mwisho, na adhabu iliyotolewa kutoka mikononi mwangu ni adhabu isiyo na mwisho, kwani bBila mwisho ndilo jina langu. Kwa hiyo—

11 Adhabu ya amilele ni adhabu ya Mungu.

12 Adhabu isiyo na mwisho ni adhabu ya Mungu.

13 Kwa hiyo, ninakuamuru wewe kutubu, na kuzishika aamri ambazo umezipokea kwa mkono wa mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, katika jina langu;

14 Na ni kwa uwezo wangu mkuu kwamba mmeyapata hayo;

15 Kwa sababu hii ninakuamuru wewe kutubu—tubu, nisije nikakupiga kwa fimbo ya kinywa changu, na ghadhabu yangu, na kwa hasira yangu, na amateso yako kuwa machungu—machungu namna gani hujui, makali namna gani hujui, ndiyo, namna gani magumu kuyavumilia hujui.

16 Kwani tazama, Mimi, Mungu animeteseka mambo haya kwa ajili ya wote, ili kwamba bwasipate kuteseka kama cwatatubu;

17 Lakini kama hawatatubu lazima awateseke hata kama Mimi;

18 Mateso ambayo yaliyosababisha Mimi mwenyewe, hata Mungu, mkuu kuliko yote, kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutoka damu kwenye kila kinyweleo, na kuteseka mwili na roho—na kutamani anisinywe kikombe kichungu, na kusita—

19 Hata hivyo, utukufu na uwe kwa Baba, na Mimi nikachukua na akukamilisha maandalizi yangu kwa wanadamu.

20 Kwa hiyo, ninakuamuru tena kutubu, nisije nikakunyenyekeza wewe kwa uwezo wangu mkuu; na kwamba aukiri dhambi zako, usije ukateseka kwa adhabu hizi ambazo nimezisema, ambazo katika udogo wake, ndiyo, hata katika kiwango kidogo ulionja wakati ule Mimi nilipomwondoa Roho yangu.

21 Na ninakuamuru wewe ausihubiri chochote bali toba, na busiyaonyeshe mambo haya kwa ulimwengu mpaka itakapokuwa hekima kwangu.

22 Kwani hao ahawaiwezi nyama sasa, bali bmaziwa lazima wapate; kwa sababu hiyo, wao ni lazima wasiyajue mambo haya, wasije wakaangamia.

23 Jifunze kwangu, na sikiliza maneno yangu; aenenda katika bunyenyekevu wa Roho yangu, na utapata camani kwangu.

24 Mimi ni aYesu Kristo; nilikuja kwa mapenzi ya Baba, na ninafanya mapenzi yake.

25 Na tena, ninakuamuru wewe, kwamba ausitamani bmke wa jirani yako; wala kutafuta maisha ya jirani yako.

26 Na tena, ninakuamuru kwamba usitamani mali yako mwenyewe, bali itoe bure kwa uchapishaji wa Kitabu cha Mormoni, ambacho kina aukweli wa neno la Mungu—

27 Ambacho ni neno langu kwa aMyunani, kwamba karibu kitaweza kwenda kwa bMyahudi, ambao kwao Walamani ni cbaki, ili waweze kuiamini injili, na wasitazamie kuja kwa dMasiya ambaye tayari amekuja.

28 Na tena, ninakuamuru kwamba itakupasa akusali kwa bsauti na pia katika moyo wako; ndiyo, mbele ya umati na vile vile sirini, katika hadhara na pia kibinafsi.

29 Na wewe autatangaza habari njema, ndiyo, uitangaze juu ya milima, na juu ya kila mwinuko, na miongoni mwa kila watu ambao utaruhusiwa kuwaona.

30 Na utafanya kwa unyenyekevu wote, aukiamini katika Mimi, usitukane dhidi ya wenye kutukana.

31 Na juu ya aimani wewe usizungumzie, bali wewe utatangaza toba na bimani juu ya Mwokozi, na condoleo la dhambi kwa dubatizo, na kwa emoto, ndivyo, hata fRoho Mtakatifu.

32 Tazama, hii ni kuu na aamri ya mwisho ambayo nitakupa wewe kuhusiana na jambo hili; kwani hili litatosha kwa matembezi yako ya kila siku, hata mwisho wa maisha yako.

33 Na mateso utapata kama utapuuza aushauri huu, ndiyo, hata maangamizo yako mwenyewe na mali yako.

34 aToa sehemu ya mali yako, ndiyo, hata sehemu ya ardhi yako, na yote isipokuwa ya kutegemeza familia yako.

35 Lipa adeni ambalo bulikubaliana na mchapishaji. Jiondoe mwenyewe kutoka kwenye cutumwa.

36 aOndoka nyumbani mwako, isipokuwa wakati wewe utakapotamani kuiona familia yako;

37 Na asema kwa uhuru na wote; ndiyo, hubiri, shawishi, tangaza bukweli, hata kwa sauti kubwa, na kwa sauti ya furaha, paza sauti—Hosana, hosana, libarikiwe jina la Bwana Mungu!

38 aOmba daima, na Mimi bnitakumwagia Roho yangu juu yako, na baraka kubwa itakuwa juu yako—ndiyo, hata zaidi kuliko kama ungelipata hazina za dunia na uozo uliomo ndani yake.

39 Tazama, unaweza wewe kusoma haya bila kufurahi na kuinua moyo wako kwa furaha?

40 Au waweza wewe kukimbia mwendo mrefu kama kiongozi kipofu?

41 Au waweza wewe kuwa amnyenyekevu na msikivu, na kujiendesha mwenyewe kwa hekima mbele zangu? Ndiyo, buje kwangu Mimi Mwokozi wako. Amina.