2011
Wamisionari Wengi Maishani Mwangu
Februari 2011


Vijana

Wamisionari Wengi Maishani Mwangu

Jumapili ya kwanza nilipohudhuria kanisa na wamisionari, niliwatambua watu ambao nilikua nao na kuwajua kutoka jamii. Nilimwona mmoja wa marafiki zangu wa dhati kutoka shuleni, makatibu wa shule za msingi na upili na msichana ambaye sikuwa mwema sana kwake wakati uliopita; na hata kijana mmoja niliyekuwa nimempenda.

Kila mmoja wa watu hawa binafsi alikuwa na athari ya kudumu kwangu. Rafiki wangu wa dhati alikuwa msichana wa uadilifu mkubwa, na kwa sababu yake nilichagua kuendelea kuchunguza Kanisa. Makatibu walionikumbuka kutoka shuleni walinisaidia kujua kuwa mimi ni muhimu. Nilijifunza kuhusu upendo wa kiungu na hisani kutoka kwa msichana aliyenikumbatia licha ya ukosefu wangu wa upole kwake wakati uliopita. Kijana niliyempenda wakati wa mapema wa ujana wangu alikuwa mfano mwema, nilitambua mwangaza wake na kutaka kuwa karibu naye.

Uzoefu huu ulinifundisha kwamba, hata kabla ya kukutana mara ya kwanza na wamisionari, Baba wa Mbinguni alikuwa amenitayarisha kupokea injili yake kupitia kwa watu aliowaweka karibu nami. Kutoka kwao nilijifunza kuwa vitu vidogo tunavyoweza kufanya vinaweza kuwa na athari kubwa. Muhimu zaidi, nilijifunza kuwa kazi ya umisionari huanza na mimi.