2011
Urejesho wa Vitu Vyote
Februari 2011


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi Februari 2011

Urejesho wa Vitu Vyote

Soma kifaa hiki, na kama inavyostahili kizungumzie pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Picha
Relief Society seal

Imani • Familia • Usaidizi

Nabii Joseph Smith aliunda Muungano wa Usaidizi wa kina Mama kama sehemu muhimu ya Kanisa. Kama urais, tunatumaini kwamba tunaweza kuwasaidia kuelewa kwa nini Muungano wa Usaidizi wa kina Mama ni muhimu kwa maisha yako.

Tunajua kuwa wanawake katika Agano Jipya walionyesha imani yao kwa Yesu Kristo na kushiriki katika kazi yake Luka 10:39 inasema kuhusu Maria “aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.” Katika Yohana 11:27 Martha anashuhudia Kristo: “Akamwambia, Naam Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.” Matendo ya Mitume 9:36, 39 inazungumzia “mwanafunzi mmoja aliitwa Tabitha… . alikuwa amejaa matendo mema. … na wajane wote wakasimama karibu naye… kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona.” Fibi, katika Warumi 16:1–2, alikuwa “mhudumu wa kanisa” na “msaidizi wa watu wengi.”

Hii mipangilio ya imani, ushuhuda na huduma iliendelea katika Kanisa la siku za mwisho, na ikarasimishwa na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Julie B. Beck, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama alifundisha, “Kama vile Mwokozi alivyowaalika Maria na Martha wa nyakati za agano jipya kushiriki katika kazi yake, wanawake katika Maongozi haya ya Mungu wana wajibu rasmi wa kushiriki katika kazi ya Bwana … Kuundwa kwa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama mnamo 1842 kulihamasisha uwezo wa pamoja wa wanawake na majukumu yao halisi kujenga ufalme wa Bwana.”1

Tunatimiza kazi yetu tunapotilia mkazo makusudi ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama: Kuzidisha imani na utakatifu wa kibinafsi, kuimarisha familia na nyumba, na kutafuta na kuwasaidia walio na mahitaji.

Nashuhudia kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama uliundwa kwa Uungu ili kuisaidia kazi ya wokovu Kila dada wa Muungano wa usaidizi wa kina Mama ana jukumu muhimu katika kutimiza kazi hii takatifu

Silvia H. Allred, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama.

Kutoka kwa Maandiko

Yoeli 2:28–29; Luka 10:38–42; Waefeso 1:10

Kutoka kwa Historia Yetu

Dada Julie B. Beck amefundisha kuwa “tunajua kupitia kwa Nabii Joseph Smith kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ulikuwa sehemu rasmi ya Urejesho.”2 Kazi ya urejesho ulianza na Ono la Kwanza mnamo 1820, na kuendelea “amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni” (M&M 98:12). Wakati Muungano wa Usaidizi wa kina Mama ulipoundwa rasmi mnamo Machi 17, 1842, Nabii aliwafundisha wanawake kuhusu sehemu yao muhimu katika Kanisa lililorejeshwa. Alisema, “Kanisa haikuratibiwa kikamilifu hadi wanawake pia waliporatibiwa.”3

Muhtasari

  1. Julie B. Beck, “Fulfilling the Purpose of Relief Society,” Liahona, Nov. 2008, 108.

  2. Julie B. Beck, “Fulfilling the Purpose of Relief Society,” 108.

  3. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 451.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Ni usaidizi gani ninaoweza kuwapa kina dada zangu mwezi huu utakaodhihirisha imani ya wafuasi wa kike wa Yesu Kristo?

  2. Ni mafundisho gani ya Injili iliyorejeshwa nitakayojifunza ambayo yataimarisha ushuhuda wangu mwezi huu?