2012
Msamaha Huleta Furaha
Oktoba 2012


Watoto

Msamaha Huleta Furaha

Rais Uchtdorf hufunza kwamba tunafaa kuwasamehe wanafamilia wetu. Ona jinsi changuzi za Joseph na Anna vile zinaathiri familia zao.

Joseph na dada yake mdogo, Anna, wanacheza pamoja. Anna ananyakua kidude cha Joseph kutoka kwake. Joesph anafaa kufanya nini?

Joseph anamkasirikia Anna. Anna analia. Mama ya Joseph anamuadhibu kwa kupingana na dada yake. Joseph anajuta kwamba amefanya uchaguzi mbaya.

Joseph anamsamehe Anna na kupata kidude kingine na kucheza nacho.Wanacheza pamoja kwa furaha. Mama yao anafurahi kwamba Joseph amekuwa mkarimu kwa dada yake na kudumisha amani katika familia. Joseph anahisi furaha kwa kuchagua kusamehe.

Baadaye, Joseph na Anna wanahitaji kumsaidia mama yao kutayarisha chakula cha jioni. Joseph hakusaidia. Anna anafaa kufanya nini?

Anna analalamika kwa mama yake. Anna ananung’unika juu ya kufanya kazi peke yake. Wakati wa chakula cha jioni kila mtu hana furaha kwa sababu ya ubishi.

Anna anamsamehe Joseph na anasaidia wakati wa chakula cha jioni. Mama yao ana shukrani kwa usaidizi wa Anna. Familia inafurahia kuwa pamoja wakati wa chakula cha jioni. Anna anahisi vyema kwamba alichagua kusamehe

Je! Chaguzi zako za kusamehe zinaathiri vipi furaha ya familia yako?