2012
Funguo Moja kwa Familia yenye Furaha
Oktoba 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Oktoba 2012

Msingi Muhimu kwa Familia yenye Furaha

Picha
Na Rais Dieter F. Uchtdorf

Mwandishi maarufu wa Kirusi Leo Tolstoy alianza riwaya Anna Karenina kwa maneno haya: “Familia zenye furaha zote zinafanana; kila familia isio na furaha inakuwa haina furaha kivyake.”1 Ingawaje mimi sina hakika ya Tolstoy kwamba furaha ya familia zote zinafanana, nimetambua kitu kimoja ambacho familia zote ni sawa sawa: zina njia ya kusamehe na kusahau upungufu wa wengine na kutafuta wema.

Wale walio katika familia zisizo na furaha, kwa upande mwingine, mara nyingi wanaona makosa, wanakuwa na kinyongo, na hawaonekani kusahau makosa yaliyopita.

“Ndio, lakini ” anza na wale wasio na furaha. “Ndio, lakini haujui jinsi anavyoniumiza mimi vibaya,” asema mmoja. “Ndio, lakini haujui jinsi huyu alivyo mbaya.” asema mwingine.

Labda wote ni sahihi; lakini hakuna yeyote.

Kuna viwango vingi vya makosa. Kuna viwango vingi ya uchungu. Lakini kile nimeona ni kwamba kila mara tunahalalisha ghadhabu yetu na kuridhisha dhamiri zetu kwa kujiambia wenyewe hadithi kuhusu dhamira za wengine ambazo zinashutumu matendo yetu kama yasiweza kusameheka na ubinafsi, hali wakati huo huo, tukikweza dhamira zetu kama halisi na maasumu.

Mbwa wa Mwana Mfalme

Kuna hadithi ya kale ya Kiwelishi kutoka katika karne ya 13 kuhusu mwana mfalme ambaye alirudi nyumbani na kumpata mbwa wake hakitiririkwa na damu usoni mwake. Huyu mtu akakimbia ndani na, kwa kushituka, akaona kwamba mvulana mchanga wake hakuwepo na susu yake ikiwa umependuliwa. Kwa ghadhabu mwana mfalme akauchomoa upanga wake na kumuua mbwa wake. Muda mfupi baadaye, akasikia kilio cha mwanawe—mtoto alikuwa hai! Kandoni mwa mtoto mchanga alilala mbwa mwitu aliyekufa. Yule mbwa, kwa kweli, alikuwa amemlinda mtoto wa mwana mfalme kutoka kwa mbwa mwitu muuaji.

Ingawaje hii hadithi ni ya tamthiliya, inaonyesha jambo fulani. Inaonyesha uwezekano kwamba hadithi hii unatuambia kuhusu kwa nini wengine wanatenda kwa njia fulani kila mara haiambatani na sababu—ambazo wakati mwengine sisi hata hatutaki kujua sababu. Tungependa afadhali tuhisi kujihalalisha wenyewe katika ghadhabu yetu hata kwenye uchungu wetu na maudhi. Wakati mwengine hiki kinyongo kinaweza kuwa kwa miezi au miaka. Wakati mwengine kinaweza kuwa kudumu maisha.

Familia Iliyogawanyika

Baba mmoja hakuweza kumsamehe mwanawe kwa ajili ya kupotoka kutoka kwa njia aliyokuwa amemfunza. Huyu mvulana alikuwa na marafiki ambao baba yake hakupendelea, na alifanya mambo mengi kinyume na kile baba alifikiria alifaa kufanya. Haya yalileta ugomvi kati ya baba na mwana, na huyu mvulana punde alipojiweza, alihama nyumbani na asirudi kamwe. Hawakuongeleshani tena.

Je! Huyu baba alihisi kujihalalisha? Labda

Je! Huyu mwana akihisi kujihalalisha? Labda

Yote ninayojua ni kwamba hii familia iligawanyika na haikuwa na furaha kwa sababu baba wala mwana hakuweza kusamehe mwenzake. Hawangeweza kuona zaidi ya kumbukumbu chungu walizokuwa nazo kuhusu kila mmoja. Walijaza mioyo yao na ghadhabu badala ya upendo na msamaha. Kila mmoja alijinyima nafasi ya kuathiri maisha ya mwenzake kwa wema. Mgawanyiko kati yao ulionekana kuwa wa kina na mpana sana kwamba kila mmoja akawa mfungwa kiroho katika kisiwa chake mwenyewe cha mhemko.

Kwa bahati nzuri, Baba yetu wa Milele aliye Mbinguni mwenye upendo na hekima alifanya njia ya kushinda ufa huu wa kiburi. Upatanisho mkuu na usio na mwisho ni tendo kuu la msamaha na suluhu. Uzito wake ni zaidi ya uelewa wangu, lakini nashuhudia kwa moyo na nafsi yangu yote juu uhalisi na uwezo wake wa msingi. Mwokozi alijitoa Mwenyewe kama fidia ya dhambi zetu. Kupitia Kwake sisi tunapata msamaha.

Hakuna Familia Iliyokamili.

Hamna yeyote kati yetu asiye na dhambi. Kila mmoja wetu hufanya makosa, ikijumuisha wewe na mimi. Sisi sote tumeshapata kuumizwa. Sisi sote tumepata kuumiza wengine.

Ni kupitia dhabihu ya Mwokozi wetu kwamba tunaweza kupata kuinuliwa na uzima wa milele. Tunapokubali njia Zake na kushinda kiburi chetu kwa kulainisha mioyo yetu, tunaweza kuleta suluhu na msamaha katika familia zetu na maisha yetu binafsi. Mungu atatusaidia sisi kuwa wenye kusamehe zaidi, kuwa tayari kutembea maili ya pili, kuwa wa kwanza kuomba msamaha hata kama jambo hailikuwa kosa letu, kutupilia mbali kinyongo cha zamani na kutokikuza tena. Shukrani ziwe kwa Mungu, ambaye alimtoa Mwanawe wa Pekee, na kwa Mwanawe, ambaye aliyatoa maisha Yake kwa ajili yetu.

Tunaweza kuhisi upendo wa Mungu kwetu kila siku. Je! Si tunafaa kujitoa zaidi kidogo kwa wenzetu kama tunavyofunzwa kwenye wimbo “Kwa Sababu Mimi Nimepewa Sana”?2 Bwana amefungua mlango kwetu ili tusamehewe. Je! Si ingekuwa sawa tu kutupilia mbali ubinasfi wetu na kiburi chetu na kuanza kufungua huo mlango iliobarikiwa wa msamaha kwa wale ambao tunaoangahika kwa ajili yao—hasa kwa wote wa familia zetu wenyewe?

Hatimaye, furaha haichomoki kutoka kwa ukamilifu bali kutoka kwa kutumia kanuni takatifu, hata kwa hatua ndogo. Urais wa Kwanza na Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili wametangaza: “Furaha katika maisha ya familia sana sana inaweza kupatikana inapojengwa kwa mafundisho ya Bwana Yesu Kristo. Ndoa na familia zenye ufanisi zimejengwa na kukuzwa katika misingi ya imani, maombi, toba, msamaha, heshima, upendo, huruma, kazi, na matendo mazuri ya maburudisho.”3

Msamaha umewekwa hapo katikati ya hizi kweli rahisi, zilizojengwa juu ya mpango wa furaha wa Baba yetu wa Mbinguni. Kwa sababu msamaha unaunganisha kanuni, unaunganisha watu. Ni funguo, hufunguao milango iliyofungwa, ni mwanzo wa njia ya uaminifu, na ni matumaini yetu bora kwa furaha yenye furaha.

Na Mungu atusaidie kuwa zaidi kidogo wa kusamehe katika familia zetu, kuwa zaidi wa kusameheana mmoja na mwingine, na labda zaidi wa kujisamehe wenyewe. Naomba kwamba sisi tuweze kupata uzoefu wa msamaha kama njia moja ya ajabu ambayo kwayo familia nyingi zenye furaha zinafanana.

Muhtasari

  1. Leo Tolstoy, Anna Karenina, trans. Constance Garnett (2008), 2.

  2. “Because I Have Been Given Much,” Hymns, no. 219.

  3. “Familia: Tamko kwa Ulimwengu,” Liahona, Nov. 2010, 129; mkazo umeongezewa.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

“Unapotayarisha kila somo, jiulize jinsi hii kanuni ilivyo kama kitu wanafamilia walipata uzoefu nacho katika maisha yao wenyewe” (Teaching, No Greater Call [1999], 171). Fikiria kuwaalika wanafamilia ili washiriki uzoefu mwema waliopata au kuona kuhusu msamaha. Zungumza juu ya huu uzoefu, ukisisitiza juu ya msamaha. Hitimisha kwa kutoa ushuhuda wa umuhimu wa kusameheana mmoja na mwengine.