2016
Moto na Masomo ya Utiifu
Oktoba 2016


Vijana

Moto na Masomo ya Utiifu

Rais Thomas S. Monson aliwahi kusema kuhusu kipindi ambacho alijifunza umuhimu wa kutii. Alipokuwa na miaka minane, familia yake walitembelea banda lao lililoko milimani. Yeye na rafiki yake walitaka kuondoa nyasi kwa ajili ya kukoka moto. Walijaribu kuondoa nyasi hizo kwa mkono, kwa kuvuta na kwa nguvu kadili walivyoweza, lakini walifanikiwa kuondoa magugu kidogo tu. Rais Monson alielezea, “Na basi kile nilicho fikiria kuwa ndio suluhisho kamili likaja katika akili yangu yenye umri wa miaka minane. Nilimwambia Danny, “Kile tunachohitaji kufanya ni kuchoma haya magugu kwa moto. Sisi tutachoma duara katika magugu!”

Hata hivyo alijua hakuruhusiwa kutumia kiberiti, alikwenda kwenye kibanda kuchukua, na yeye na Danny waliwasha moto mdogo kwenye zile nyasi. Walitegemea ungezima wenyewe, lakini badala yake ulikua mkubwa na kuwa moto wa hatari. Yeye na Danny walikwenda kuuzima, na mara watu wazima walikuwa wakikimbia kwenda kuuzima moto kabla haujaifikia miti.

Rais Monson aliendelea, Danny na mimi tulijifunza masomo magumu kadhaa lakini muhimu siku hiyo---sehemu kuu ambayo ilikuwa ni umuhimu wa utiifu. (Ona “Utiifu Huleta Baraka,” Liahona Mei 2013, 89, 90.)

Kama ilivyokuwa kwa Rais Monson, umewahi kujifunza somo la utiifu kwa njia ngumu? Ni malengo gani unayoweza kuyaweka ili kujiweka mwenyewe salama kupitia utiifu hapo baadaye?