2016
Familia ni Mpango wa Mungu.
Oktoba 2016


Ujumbe wa Ualimu wa Kutembelea, Oktoba 2016

Familia ni Mpango wa Mungu

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute maongozi kujua kitu cha kufundisha. Je, kuelewa “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” kutazidisha vipi imani yako katika Mungu na kubariki wale unaowachunga kupitia ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Imani, Familia, Usaidizi

“Katika maneno ya [Wimbo wa Watoto], ‘The Family Is of God,’ … tunakumbushwa juu ya mafundisho mazuri,” alisema Carole M. Stephens, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Hatujifunzi tu kwamba familia ni ya Mungu bali pia kwamba sisi ni sehemu ya familia ya Mungu. …

“… Mpango wa Baba kwa watoto wake in mpango wa upendo. Ni mpango wa kuwaunganisha watoto Wake—familia Yake—pamoja Naye.”

Mzee L. Tom Perry (1922–2015) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Sisi pia tunaamini kwamba familia za kitamaduni zenye nguvu siyo tu asasi muhimu ya jamii imara, uchumi imara, na utamaduni imara wa maadili bali pia kwamba ni asasi muhimu za milele na za ufalme, na serikali ya Mungu.

Tunaamini kwamba shirika na serikali ya mbinguni itajengwa kwa misingi ya familia na jamaa.”2

Kila mtu, haijalishi hali yao ya ndoa au idadi ya watoto, anaweza kuwa mtetezi wa mpango wa Bwana ambao umeelezwa katika tangazo la familia” alisema Bonnie L. Oscarson, Rais Mkuu wa Wasichana. Ikiwa ni mpango wa Bwana, unapaswa kuwa mpango wetu pia!3

Maandiko ya Ziada

Mafundisho na Maagano 2:1–3; 132:19

Mafundisho ya Familia

Dada Julie B. Beck, aliyekuwa Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alifundisha kwamba teolojia ya familia kulingana na Uumbaji, Anguko, na Upatanisho wa Yesu Kristo:

Uumbaji wa dunia uliwezesha kupatikana kwa mahali ambapo familia zingeweza kuishi. “Mungu alimwumba mwanaume na mwanamke ambao walikuwa nusu mbili muhimu za familia. Ilikuwa ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kwamba Adamu na Hawa waunganishwe na kutengeneza familia ya milele.

“… Anguko liliwezesha wao kupata wana na mabinti.

“Upatanisho wa [Kristo] unaiwezesha familia kuunganishwa pamoja milele. Unaruhusu familia kuwa na makuzi ya milele na kukamilika. Mpango wa furaha, pia unaitwa mpango wa wokovu, ulikuwa ni mpango uliowekwa kwa ajili ya familia. …

“… Haya ndiyo yalikuwa mafundisho ya Kristo. … Bila ya familia, hakuna mpango; hakuna sababu ya maisha ya duniani.”4

Muhtasari

  1. Carole M. Stephens, “Familia ni ya Mungu,” Liahona, Mei 2015, 11, 13.

  2. Ulimwengu,” Liahona, Mei 2015, 41.

  3. Bonnie L. Oscarson, “Defenders of the Family Proclamation,” Liahona, Mei 2015, 15.

  4. Julie B. Beck, “Teaching the Doctrine of the Family,” Liahona, Machi 2011, 32, 34.

Zingatia Hili

Kwa nini familia ni asasi muhimu sasa na milele?