2021
Akina Dada wa Rollins Okoa Siku!
Juni 2021


“Akina Dada wa Rollins Okoa Siku!” Rafiki, Juni 2021

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki June 2021

Akina Dada wa Rollins Okoa Siku!

Picha
Joseph Smith akiangalia makaratasi

Vielelezo na Apryl Stott

Yesu Kristo alimweleza Nabii Joseph Smith vitu vingi muhimu kutusaidia. Kanisa lilianzisha kiwanda cha kupiga chapa kuchapisha maneno ya Yesu. Kwa njia ile watu watakuwa na uwezo wa kuyasoma.

Picha
wanaume wakiyatupa makaratasi

Siku moja, kundi la wanaume wenye hasira walikuja. Waliharibu kiwanda cha kupiga chapa. Walitupa kurasa za maandiko nje kwenye mtaa.

Picha
wasichana wakikimbia na makaratasi

Dada wawili walioitwa Mary Elizabeth na Caroline Rollins waliona kile kilichotokea. Walikimbia na walikusanya karatasi kwenye mikono yao.

Picha
wasichana wakijificha ndani ya shamba la mahindi

Wasichana walijificha ndani ya shamba la mahindi mpaka wanaume walipoondoka. Walikuwa wameokoa maandiko! Maandiko hayo baadaye yalikuwa sehemu ya Mafundisho na Maagano.

Picha
msichana na bibi wakisoma maandiko ndani ya basi

Ninaweza kusoma maandiko. Ninaweza kuwa jasiri na kusimama wima kwa ajili ya kile ninachoamini.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Naweza Kuwa Jasiri.

Picha
mtoto akipata chanjo

Ni nini kinachokusaidia kuwa jasiri?