2021
Kupata Nguvu ya Kusamehe
Juni 2021


“Kupata Nguvu ya Kusamehe,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 10-11.

Njoo, Unifuate

Kupata Nguvu ya Kusamehe

Bwana ametuamuru kuwasamehe wengine. Atatusaidia kuweka amri zake, ikijumuisha hii.

Mafundisho na Maagano 64:10

Picha
mwanamke akimtazama mtu fulani anayemnyooshea mkono

Kielelezo na Jim Madsen

Je, kuna baadhi ya amri zinazoonekana ngumu kuziweka kuliko zingine?

Hii hapa ni mojawapo ambayo inawaogofya watu wengi: “Mimi, Bwana, nitamsamehe yule nitakaye kumsamehe, lakini ninyi mnatakiwa kuwasamehe watu wote” (Mafundisho na Maagano 64:10).

Ngoja. Tunapaswa kumsamehe kila mtu aliyetukosea? Je, hiyo hata inawezekana?!

Ni kitu kimoja kumsamehe mtu kwa kusema kitu cha ufidhuli kwako au kwa kuvunja maadili ya ustaarabu wa mezani wakati mlo. Lakini vipi kuhusu vidonda vya kina? Makosa hayo makubwa ambayo yanaweza kuvuruga au hata kubadili uelekeo wa maisha yetu?

Wakati mwingine uwezo wa kumsamehe mtu ambaye ametuumiza vibaya sana unaweza kuhisi zaidi ya uwezo wetu.

Hizi hapa ni habari nzuri: Kwa msaada wa Yesu Kristo, kamwe hatuna kikomo kwa kile tunachoweza kukifanya sisi wenyewe.

Msaada Aliouhitaji

Mkristo mwenye kumcha Mungu kutoka Uholanzi aliyeitwa Corrie ten Boom aligundua moja kwa moja uwezo wa kumwomba Mungu kumsaidia kumsamehe mtu.

Yeye na dada yake Betsy walikuwa wamefungwa gerezani katika kambi za mateka wa vita wakati wa Vita ya Dunia II. Corrie na wengine walivumilia uonevu mbaya sana kutoka kwa walinzi wa gereza la Wanazi. Dada yake Betsy hata alikufa kutokana na uonevu ule. Corrie alipona.

Baada ya vita, Corrie aligundua uwezo wa kuponya kwa kuwasamehe wengine. Mara kwa mara alishiriki ujumbe wake katika vikao vya umma. Baadaye siku moja maneno yake hatimaye yalijaribiwa.

Kufuatia mhadhara, Corrie alifuatwa na mmoja wapo wa walinzi wa gereza katili sana kutoka kambi zile.

Alimwambia Corrie kwamba amekuwa Mkristo tangu wakati wa vita na ametubu vitu vyote vibaya alivyovifanya kama mlinzi wa gereza.

Alimnyooshea mkono wake na kusema, “Utanisamehe?”

Licha ya yote aliyojifunza na kushiriki kuhusu kusamehe wengine, Corrie hakuweza kukubali mkono huu mahususi wa mwanaume huyu na kumsamehe—sio kwake mwenyewe, kwa vyovyote vile.

Baadaye aliandika, “Pamoja na kuwa na hasira, mawazo ya kulipiza kisasi yaliongezeka, nikaona dhambi zao. … Bwana Yesu, niliomba, nisamehe na nisaidie nimsamehe yeye.

Nilijaribu kutabasamu, [na] nilijitahidi kuinua mkono wangu. Sikuweza. Sikujisikia chochote, hata chembe ndogo ya ukunjufu au upendo. Na kisha tena nilivuta pumzi ya sala ya kimya. Yesu, Siwezi kumsamehe huyu. Nipe msamaha Wako.

“Nilipoushika mkono wake kitu cha ajabu kikatokea. Toka mabegani mwangu hadi mikononi kuelekea viganjani, mkondo ulikuwa kutoka kwangu kwenda kwake, wakati moyoni mwangu kukaibuka upendo kwa mgeni huyu ambao karibu ulinishinda.

“Na hivyo nikagundua kwamba sio juu ya msamaha wetu tena kuliko juu ya wema wetu kwamba bawaba za uponyaji wa ulimwengu zinategemea, bali kwa njia Zake. Anapotuambia tuwapenda adui zetu, Anatupa, pamoja na amri, upendo wenyewe.”1

Mungu yupo pale kukusaidia kuweka amri Zake, pamoja na amri ya kusamehe—hata inapokuwa ni vigumu. Anaweza kukusaidia kama vile alivyomsaidia Corrie ten Boom.

Uponyaji Unaostahili

Maisha ukanganya. Yana fujo. Na kabisa yamejaa watu wenye uhuru wa kujiamulia waliopewa—na Mungu.

Muda wote wa nyakati hizo wakati mtu anafanya uchaguzi ambao unakusababishia maumivu makubwa—au hata kwa bahati mbaya unafanya hivyo— unaweza kupokea uwezo wa uponyaji unaposali kwa ajili ya msaada na kujitahidi kusamehe.

Kuwasamehe wengine kunaleta uponyaji kwa nafsi yako. Kwa msaada wa Mungu, unapomsamehe mtu ambaye amekukosea, unatua mzigo wenye usumbufu mkubwa kutoka mabegani mwako ambao unakuzuia. Hata wakati njia ya kwenda kwenye uponyaji wa kweli inaonekana mgumu, pamoja na Mungu, kamwe hutahitaji kuitembea peke yako.

Muhtasari

  1. Corrie ten Boom, The Hiding Place (1971), 215.

  2. Jeffrey R. Holland, mkutano mkuu wa Oktoba 2018 (Ensign, au Liahona, Novemba 2018, 79).