2021
Uungu Ni Nini?
Juni 2021


“Uungu ni nini?,” Liahona, Juni 2021

Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Liahona , June 2021

Uungu Ni Nini?

Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu ni viumbe vitatu tofauti vyenye kusudi moja.

Picha
Ono la Kwanza

Kila kitu kutoka Ono la Kwanza, na Jon McNaughton

Mhariri wa gazeti hapo mwanzo alimwuliza Nabii Joseph Smith waumini gani wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho waliamini. Kwa kujibu, nabii aliandika kauli 13 za imani tunazoziita Makala ya Imani. Kauli ya kwanza inasema, “Tunaamini katika Mungu, Baba wa Milele, na katika Mwanae,Yesu Kristo, na katika Roho Mtakatifu” (Makala ya Imani 1:1). Hawa watatu wanaunda kile tunachokiita Uungu.

Mungu, Baba wa Milele

Mungu ana mwili mkamilifu, mtukufu, usiokufa wa nyama na mifupa. Yeye ni Baba wa roho zetu. Anampenda kila moja wa watoto Wake kikamilifu. Mungu ni mkamilifu, ana nguvu zote, na anajua kila kitu. Yeye ni mwenye haki, mwenye huruma, na mpole. Tuliishi kama roho na Mungu kabla hatujazaliwa. Alituleta duniani kujifunza na kukua. Matumaini makubwa ya Mungu kwa ajili ya kila mmoja wa watoto Wake ni kurudi kuishi pamoja Naye tena baada ya kufa kwetu. Mungu anatufundisha kwamba lazima tumfuate Yesu Kristo ili turudi kwenye uwepo wa Mungu.

Picha
Yesu Kristo Akihubiri katika Ulimwengu wa Roho

Kristo Akihubiri katika Ulimwengu wa Roho, na Robert T. Barrett

Yesu Kristo

Yesu Kristo pia ana mwili mkamilifu, mtukufu, wa nyama na mifupa. Yeye ni Mwana mzaliwa wa kwanza wa Mungu. Kabla hatujazaliwa, Mungu alimchagua Yeye kuwa Mwokozi wetu. Hii inamaanisha Yesu alikuja duniani kuwa mfano kwa ajili yetu, kufundisha Injili, kulipia dhambi zetu, na kutuokoa kutoka kwa kifo. Kwa sababu ya Yesu, tunaweza kusamehewa dhambi zetu tunapotubu. Yesu Kristo pia aliteseka mambo mengi ili kwamba angeweza kuelewa na kutusaidia. Yesu Kristo alikufa na kisha kuishi tena, kufanya iwezekane kwa kila mtu kuishi tena.

Picha
mazishi ya Kristo

Picha kutoka Getty Images

Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu ni mshiriki mmoja wa Uungu ambaye hana maumbile ya kimwili. Yeye ni roho. Roho Mtakatifu anaweza kuwasiliana moja kwa moja na roho zetu. Anashuhudia kwetu kwamba Mungu ni wa kweli na kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wetu. Roho Mtakatifu anatenda kama mjumbe wa Mungu kutupa sisi hisia za upendo, mwongozo, au faraja. Tunapobatizwa na kuthibitishwa, tunapokea karama za Roho Mtakatifu. Baada ya ubatizo wetu, Roho Mtakatifu anaweza siku zote kukaa nasi tunapotunza amri za Mungu.

Picha
Ono la Kwanza

Ono la Kwanza, na Walter Rane

Ono la Kwanza la Joseph Smith

Baada ya muda watu wamechanganyikiwa kuhusu Uungu. Watu hawakubaliani kuhusu juu ya jinsi Mungu, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu walivyo. Hii ni sababu moja kwa nini Ono la Kwanza ambalo Joseph Smith alilipata lilikuwa la muhimu sana. Aliona kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wana miili na viumbe wawili tofauti.

Picha
Kusikiliza

Kusikiliza, na Michael Jarvis Nelson

Tofauti lakini wamoja

Maandiko na manabii wa sasa wanatufundisha kwamba Mungu, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu ni viumbe tofauti wenye lengo moja: maisha yetu ya kufa na uzima wa milele (ona Musa 1:30). Kama washiriki wa timu moja, wanafanya kazi pamoja kutusaidia kila siku. Tunaweza kujihisi kuwa karibu Nao zaidi tunapotubu dhambi zetu na kuchagua yaliyo sahihi.

Maandiko kuhusu Uungu