2021
Ukuhani wa Mungu
Agosti 2021


“Ukuhani wa Mungu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Agosti. 2021, 20–21.

Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Agosti 2021

Ukuhani wa Mungu

Mafundisho na Maagano 84

Kile kila kijana anapaswa kujua juu ya ukuhani na uhusiano wao kwenye ukuhani huo.

Picha
kijana

Je, umewahi kuona jinsi inavyoweza kutatanisha wakati neno moja linatumiwa kwa njia mbili? Kwa mfano, kwa Kiingereza neno dunia linahusu sayari tunamoishi na udongo chini ya miguu yetu. Maana zote mbili ni sahihi, lakini unachomaanisha unapotumia neno hilo inategemea na kile unachozungumza kwa wakati huo. Ili kuifanya iwe ya kutatanisha zaidi, wakati dunia inamaanisha sayari yetu, pia inajumuisha wazo la udongo kwa sababu udongo uko kwenye sayari.

Kufafanua Neno Ukuhani

Neno moja tunalotumia katika Kanisa kwa njia mbili ni ukuhani. Neno linahusiana na nguvu na mamlaka kamili ya Mungu. Hata hivyo, pia tunatumia neno ukuhani kwa njia ndogo zaidi—kurejelea “nguvu na mamlaka ambayo Mungu huwapa wenye ukuhani waliowekwa wakfu kutenda katika mambo yote muhimu kwa wokovu wa watoto wa Mungu.”1

Ukuhani uliotunukiwa kwa mwanadamu sio nguvu zote za Mungu. Jedwali lifuatalo linaelezea hili.

Katika jedwali hili unaona mifano ya nguvu za Mungu, ambazo hazina mwisho na hazina mipaka. Ndani ya hayo, unaona pia mifano ya nguvu na mamlaka ya ukuhani wa Mungu ambao Yeye huutunuku, au huwapa, watu wanaostahili kuhudumu katika Kanisa la Kristo.

Mifano ya Mamlaka ya Ukuhani katika Maisha Yako

Baraka zote za ukuhani zinapatikana kwa binti na wana wote wapendwa wa Baba wa Mbinguni. Orodha ya pili inawakilisha baraka ambazo huja kwako kupitia yule aliye na funguo za ukuhani au amepewa mamlaka ya ukuhani.

Huu ndio utaratibu ambao Mungu ameweka kwa ajili ya mpangilio na usimamizi wa Kanisa Lake duniani. Mifano mingine ya mamlaka ya ukuhani wa Mungu ni pamoja na rais wa akidi ya mashemasi au walimu ambaye ana funguo za kuongoza kazi ya akidi yake, baraka za baba zinazotolewa nyumbani, na ibada na maagano ya hekaluni.

Waume, Wanawake na Ukuhani

Ingawa kutawazwa kwenye ofisi ya ukuhani kunafanywa kwa wanaume tu, Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, ameelezea kanuni muhimu: “Ukuhani ni nguvu na mamlaka ya kiungu yanayoshikiliwa kwa amana ili kutumiwa kwa kazi ya Mungu kwa faida ya Watoto Wake wote. Ukuhani siyo wale waliotawazwa kwenye ofisi ya ukuhani au wale wanaotumia mamlaka yake. Wanaume wanaoshikilia ukuhani wao siyo ukuhani. … Hatupaswi kutaja wanaume waliotawazwa kama ni ukuhani.2

Ingawa wanawake hawatawazwi kwenye ukuhani, Rais Russell M. Nelson alielezea, “unapoitwa kutumikia katika wito chini ya uongozi wa yule aliye na funguo za ukuhani … unapewa mamlaka ya ukuhani kufanya kazi katika wito huo.”3 Mifano kadhaa ya hii ni pamoja na urais wa madarasa ya Wasichana, akina dada wamisionari wakihubiri injili, viongozi katika kata na vigingi ambao wametengwa kwa ajili ya kufundisha na kuongoza, na wafanyakazi wa ibada katika hekalu.

Nguvu ya Ukuhani Humbariki Kila Mmoja

Baraka ambazo nyinyi vijana wa kiume na wa kike hupokea ni zenu kupitia maagano mnayofanya wakati wa ubatizo na maagano mtakayofanya hekaluni. Hata kama huna mwenye ukuhani katika nyumba yako, bado unaweza kubarikiwa na nguvu ya ukuhani wa Mungu maishani mwako unapotunza maagano uliyoyafanya na Yeye (ona 1 Nefi 14:14).

Tunapoishi kulingana na maagano yetu, tunapokea baraka ambazo zinatuimarisha na kutubariki. Tunakualika utafakari baraka za ukuhani katika maisha yako—baraka zinazokuja kwa sababu ya nguvu ya Mungu isiyo na mwisho ya ukuhani na zile zinazokuja hasa kupitia mamlaka ya ukuhani ambayo hutunukiwa na kutolewa katika Kanisa la Mungu.

Muhtasari

  1. Dale G. Renlund na Ruth Lybbert Renlund, Ukuhani wa Melkizedeki: Kuelewa Mafundisho, Kuishi Kanuni (2018), 11.

  2. Dallin H. Oaks, “Ukuhani wa Melkizedeki na Funguo Zake,” mkutano mkuu wa Apr. 2020 (Ensign au Liahona, Mei 2020, 69).

  3. President Russell M. Nelson, “Hazina za Kiroho,” Okt. 2019 mkutano mkuu (Ensign au Liahona, Nov. 2019, 78).