2021
Neno la Hekima
Agosti 2021


“Neno la Hekima,” Rafiki, Agosti. 2021.

Ujumbe wa Kila Mwezi wa Gazeti la Rafiki Agosti 2021

Neno la Hekima

Picha
Joseph Smith akifundisha kikundi cha wanaume

Joseph Smith alifanya mikutano ili kuwafundisha watu kuhusu injili. Wakati mwingine wanaume walivuta na kutafuna tumbaku.

Picha
Joseph na Emma Smith

Hili lilimtia wasiwasi Emma Smith. Moshi na tumbaku vilisababisha tatizo kubwa, na haikuonekana sawa. Emma na Joseph walijiuliza jinsi Mungu alivyohisi kuhusu hili.

Picha
Joseph Smith akisali

Joseph alisali na Bwana akajibu. Bwana aliwaonya waumini wa Kanisa kuhusu kuvuta sigara na tumbaku. Alisema kuwa si nzuri kwa miili yetu. Pia aliwaonya kuhusu kunywa chai, kahawa na pombe.

Picha
mboga

Mungu alisema tule matunda, mboga za majani na vyakula vingine vyenye afya. Tunayaita mafundisho haya Neno la Hekima.

Picha
Msichana akila

Ninaweza kuishi Neno la Hekima. Baba wa Mbinguni atanibariki ninapoutunza mwili wangu.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Ninaweza Kuutunza Mwili Wangu

Picha
watoto wanaruka kamba

Unafanya nini ili kuutunza mwili wako?

Bonyeza kwenye picha ili kupakua.

Kielelezo na Apryl Stott