2021
Jambo la Kutegemea Unapopokea Kibali Chako chenye Ukomo
Oktoba 2021


NJIA YANGU YA AGANO

Jambo la Kutegemea Unapopokea Kibali Chako chenye Ukomo

Kama umejiunga na Kanisa au kurejea Kanisani hivi karibuni, viongozi wako au marafiki zako wanaweza kukualika kujiandaa kupokea kibali cha hekaluni chenye ukomo.

Kupokea kibali cha hekaluni chenye ukomo wa matumizi ni wakati wa kufurahisha kwa waumini wengi wapya na vijana ndani ya Kanisa.  Wakati wa mahojiano na Askofu wako, atakuuliza maswali yanayofanana na yale uliyoulizwa kwa ajili ya ubatizo wako. Haya hujumuisha maswali kuhusu utiifu wako wa amri na ushuhuda wako wa injili. Unapopokea kibali chako, unaweza kupanga safari ya hekaluni pamoja na familia yako na rafiki zako kwenye kata.

Alipoulizwa angesema nini kwa mtu ambaye ana wasiwasi kuhusu kuhudhuria hekaluni kwa mara ya kwanza, Mosa Moloi kutoka Tawi la Cosmo City huko Johannesburg, Afrika Kusini alisema, “hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Kuna amani ndani ya nyumba ile—hekalu. Hofu zako zote na majaribu hufanywa kuwa rahisi hekaluni. Hekalu ni mahali penye utukufu, amani . . . mahali salama au jengo salama unaloweza kupata kwenye dunia hii. Sote tunakaribishwa. Mazingira yanaweza kutusukuma kutoka kwenye kuwa sisi na kuwa kwenye umoja na Baba yetu wa Mbinguni. Hekalu ni dawa, hospitali kwa ajili ya nafsi zetu ambapo nuru zetu hutoka kwenye kufifia kuwa nuru ipitayo kipimo. ‘Usiogope kwani Bwana yu nawe’ (Isaya 41:10).”

Kibali chenye ukomo wa matumizi kinakuruhusu kuhudumu katika ubatizo wa hekaluni na kufanya ibada za ubatizo na kuthibitishwa kwa ajili ya wanafamilia wako waliokwisha fariki pamoja na watu wengine ambao wamefariki. Hekalu hutoa mavazi na taulo za ubatizo kwa ajili ya matumizi yako. Kila mtu ana kabati lake na chumba chake mwenyewe kwa ajili ya kubadilishia mavazi ya kanisani ili kuvaa mavazi meupe.

Mosa anakumbuka hisia zake wakati alipokwenda hekaluni kwa mara ya kwanza; “Mara ya kwanza nilipokwenda hekaluni na kuweza kushiriki katika ibada za kanisa, ilikuwa siku isiyosahaulika kamwe. Sikuweza kuelezea furaha niliyokuwa nayo wakati ambapo niliweza kubatizwa kwa ajili ya wafu. Ilijaza moyo wangu kwa hisia nzuri kwamba ningeweza kuwasaidia wale ambao hawakupata fursa ya kuwa waumini wa kanisa au kubatizwa na kuujua ukweli. . . . Nilihisi roho yuko pamoja nami.”

Kuna njia ambazo kwazo unaweza kujitayarisha kuingia kwenye Nyumba ya Bwana kwa mara ya kwanza. Nabii wetu, Russell M. Nelson amesema, “napenda kupendekeza kwamba waumini wanaokwenda hekaluni kwa mara ya kwanza wasome aya fupi zilizofafanuliwa katika Kamusi ya Biblia zilizoorodheshwa chini ya mada saba:‘Paka Mafuta,’ ‘Upatanisho,’ ‘Kristo,’ ‘Agano,’ ‘Anguko la Adamu,’ ‘Dhabihu,’ na ‘Hekalu.’ Kufanya hivyo kutaleta msingi imara.”1

Kuwa mwenye kustahili kuingia kwenye Nyumba ya Bwana ni baraka kuu katika maisha yako. Unaweza kupokea kibali chako chenye ukomo wa matumizi mwanzoni mwa kalenda ya mwaka pale ambapo unafikisha miaka 12. Wanaume lazima wapokee Ukuhani wa Haruni kabla ya kuingia hekaluni. Unaweza kuhitaji kupiga simu mapema ili kuweka miadi hekaluni. Waombe familia yako au viongozi wa kanisa wakusaidie kuwafikia wafanyakazi wa hekaluni.

Rais Nelson pia amesema, “Kwa sababu hekalu ni nyumba ya Bwana, viwango vya kuingia vinawekwa na Yeye. Mtu huingia kama mgeni Wake. Kuwa na kibali cha hekaluni ni fursa adhimu na ishara ya kushikika ya utiifu kwa Mungu na kwa manabii Wake.”

Unapokuja kuabudu na kuhudumu hekaluni, maisha yako yatajazwa amani.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Personal Preparation for Temple Blessings,” Liahona, July 2001, 33.