2021
Oktoba 1991: Kuwekwa Wakfu kwa Uganda, Kenya na Zimbabwe
Oktoba 2021


MWEZI HUU KWENYE HISTORIA YA KANISA

Oktoba 1991: Kuwekwa Wakfu kwa Uganda, Kenya na Zimbabwe

Mnamo mwishoni mwa Oktoba 1991, Mzee James E. Faust (1920–2007) wa Akidi ya Kumi na Wawili aliziweka wakfu Uganda, Kenya na Zimbabwe kwa ajili ya kuhubiri injili na uanzishwaji wa Kanisa.

Mnamo Oktoba 23, Mzee Faust, akiwa amesindikizwa na Mzee Richard P. Lindsay (1926–2010) wa Sabini, aliyehudumu kama rais wa Eneo la Afrika, aliiweka wakfu Uganda akiwa katika mji mkuu, Kampala. Mapema mwaka huu, Uganda ilikuwa imeruhusu hadhi rasmi ya Kanisa.

Katika sala ya kuweka wakfu, Mzee Faust alimsihi Bwana kwamba katika nchi ya Uganda kungekupo “wingi wa jamii yenye amani ili kwamba wote wa watoto wako katika nchi hii waweze kuabudu kulingana na dhamiri zao wenyewe.”

Siku iliyofuata, Oktoba 24, Mzee Faust, Mzee Lindsay na Rais Larry Brown wa Misheni ya Kenya Nairobi walisafiri kwenda Nairobi, Kenya, ambapo zaidi ya waumini mia moja wa Kanisa walikusanyika kwa ajili ya shughuli ya nje.

Katika sala ya kuweka wakfu, Mzee Faust alisema, “Tunaitambua hii kama nchi iliyobarikiwa.” Sala ilijumuisha marejeleo ya uzuri wa Kenya, fahari na maisha tele ya mimea na wanyama.

Pia aliomba kwamba Waumini waweze kupata hekalu—ombi ambalo lilijibiwa mnamo Aprili 2017 wakati Rais Thomas S. Monson (1927–2018) alipotangaza kwamba kutakuwa na hekalu litakalojengwa Nairobi.

Mnamo Oktoba 25, Mzee Faust na Mzee Lindsay walikutana na Rais wa Misheni ya Zimbabwe Harare Vern Marble kwa ajili ya kuiweka wakfu Zimbabwe.

“Kabla ya mkutano, Watakatifu wa Zimbabwe walikuwa wakifunga na kusali kwa ajili ya mvua,” Mzee Lindsay alisema. “Wakati sala ya kuweka wakfu ya Mzee Faust ilipomalizika, mvua ya taratibu ilianza kunyesha na iliongezeka kwa siku kadhaa baada ya hapo.”