2021
Desemba 2000: Kitabu cha Mormoni Kinapatikana kwa Kiamhariki, Ki-Isixhosa
Desemba 2021


Mwezi huu Katika Historia ya Kanisa

Desemba 2000: Kitabu cha Mormoni Kinapatikana kwa Kiamhariki, Ki-Isixhosa

Mnamo Desemba 2000, tafsiri za Kitabu cha Mormoni katika lugha ya Amharic (inayozungumzwa Ethiopia na Eritrea) na isiXhosa (inayozungumzwa Afrika Kusini), zilikamilika kuchapishwa kwa mara ya kwanza.

“Leo nimekuwa muumini wa kwanza wa Kiethiopia kupokea Kitabu cha Mormoni katika lugha ya Amharic na nina furaha sana,” alisema Gemechu Wariyo Goja, rais wa tawi la Ethiopia Addis Ababa, akizungumza mnamo January 2001. “Wakati nilipogawa nakala za mwanzo kwa waumini niliofanya nao kazi katika kutafsiri kitabu, kila mmoja alishangilia na kurukaruka. Punde tu nikaleta nakala yangu nyumbani na familia yangu kwa shauku ikakusanyika kuzunguka kitabu, wakisomeana kwa lugha ya Amharic. Kinavutia.”

Mapema mwaka huo huo Kitabu cha Mormoni kilitafsiriwa kwa Kiswahili, ikiruhusu waumini wa Kanisa kote katika Afrika Mashariki kusoma kitabu kwa lugha yao. Huko Tanzania, Rais William Gideme wa tawi la Chang’ombe anasema, “Hatimaye ninaweza kusoma Kitabu cha Mormoni kwa familia yangu yote nikiwa na uelewa kamili. Nina shukrani nyingi.”

Mnamo Desemba 2000, jumla ya idadi ya tafsiri za lugha zilizowahi kukamilika ilifikia historia ya lugha 100. Sitini na moja kati ya hizi ni tafsiri zilizokamilika za Kitabu cha Mormoni, 39 ni tafsiri za sura zilizochaguliwa. Waumini wengi wa Kanisa Afrika sasa wanapata uzoefu wa shangwe ya kusoma Kitabu cha Mormoni katika lugha zao wenyewe.

Tafsiri ya Kitabu cha Mormoni kwa lugha nyingi pia inaahidi kuongeza mafanikio ya umisionari katika maeneo ambapo kitabu hakikuwepo kwa wachunguzi hapo kabla. Mmisionari mmoja anayetumikia Ethiopia alimwambia Rais Gemechu, “Tunakwenda kuwa na shughuli nyingi sasa.” —Julie Brough, Mmisionari wa Historia ya Kanisa Eneo la Kati mwa Afrika