2022
Mshauri wa Taasisi wa Eneo
Februari 2022


UJUMBE WA KIONGOZI WA ENEO HUSIKA

Mshauri wa Taasisi wa Eneo

Ni heri kutoa kuliko kupokea.

Kama mtoto, daima nilivutiwa na uwezo wa wamisionari wa kushiriki injili kwa urahisi na kwa ufanisi. Baadaye, nilipokuja kuwa mmoja wao, nilipata uzoefu wa nguvu ya ushuhuda binafsi na kushuhudia miujiza ikifanywa na kazi hii kuu. Lakini hakika, ningeweza kusema, ilikuwa ni nyumbani, nikiwa na wazazi na jamaa zangu, kwamba uzoefu huu ulikuwa wenye nguvu zaidi.

Katika maisha yake, baba yangu alikuwa na uhusiano maalum na Bwana. Na, akiwa amehudumu kwa miaka mingi ndani ya Kanisa kama kiongozi, mwalimu wa seminari na chuo, alikuwa amepata uzoefu wa jinsi ya kushiriki injili. Nakumbuka alikuwa akiandaa shughuli na/au desturi kama vile kuwaalika majirani kwenye jioni yetu ya familia na shughuli zingine. Na katika shughuli hizi, angesikika akishiriki injili na kutoa ushuhuda wake. Nikiwa nimehamasishwa na mfano wake, hii ilikuwa ndiyo njia yetu ya maisha. Mara kadhaa, kwa msaada wa wamisionari, tumekuwa vyombo mikononi mwa Bwana kuhusu mchakato wa uongofu kwa ajili ya baadhi ya watoto wake ambao bado ni waumini wa Kanisa hivi leo.

Ninathamini uzoefu huu ambao umeniruhusu kuelewa kuhudumu katika uzuri wake wote na urahisi wake, hivyo kupata maarifa ya thamani ya nafsi kwa kutumia mafundisho yaliyojaa hekima yaliyo katika M&M 18:10, 15: “Kumbuka thamani ya nafsi ni kubwa mbele za Mungu”, “Na kama itakuwa kwamba utafanya kazi siku zako zote katika kutangaza toba kwa watu hawa, na kuleta, japo iwe nafsi moja kwangu, shangwe yako itakuwa kubwa jinsi gani pamoja naye katika ufalme wa Baba yangu!” Hivyo, Ninaweza kuthibitisha kwamba ninaelewa hisia za Paulo anaposema “Ni heri kutoa kuliko kupokea”1.

Kupitia uzoefu binafsi na wenye nguvu, ninajua kwamba kupeleka injili kote duniani, kama vile kwa jirani mtaa wa pili, huleta baraka nyingi katika maisha yetu na katika maisha ya wanafamilia wetu. Kisha, tunaweza kuelewa hisia za Lehi ambaye, baada ya kula tunda, alianza kutamani kwamba familia yake na wengine pia waje wale tunda.2 Kama kwa uzuri ilivyoelezewa kwa maneno ya Wimbo wa Kanisa Na. 294, “Mungu Anatabasamu kwa Furaha Tele”3. tunapotimiza jukumu hili kwa dhati, uaminifu na kwa hisani”. Katika jina la Bwana Yesu Kristo, Amina!

Muhtasari

  1. Ona Matendo ya Mitume 20:35.

  2. Ona 1 Nefi 8:12.

  3. “Love at Home,” Hymns, #294.