2022
Majukumu ya Urais wa Eneo
Agosti 2022


Dondoo za Kitabu cha Maelezo

Majukumu ya Urais wa Eneo

Kama umesoma kuhusu Urais mpya wa Eneo, unaweza kujiuliza hicho ni kitu gani. Kitabu cha Maelezo ya Jumla kinatueleza zaidi kuhusu wenye ukuhani hawa ambao husimamia Kanisa katika ngazi ya eneo.

“Kanisa limepangiliwa katika maeneo ya kijiografia yaliyoenea ulimwenguni kote.”1

“Kanisa limepangiliwa katika maeneo ya kijiografia yaliyoenea ulimwenguni kote. Katika kila eneo, Sabini MKuu mwenye Mamlaka anapangiwa na Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kutumikia kama Rais wa Eneo. Washauri wawili, ambao ni Sabini Wakuu Wenye Mamlaka au Sabini wa Eneo, wanapangiwa kumsaidia rais.

Urais wa Eneo unasimamia na kushauriana na marais wa kigingi na misheni katika eneo. Pia wanawasaidia marais wa hekalu pamoja na matroni wa hekalu.

Washiriki wa Urais wa Eneo husafiri ndani ya eneo walilopangiwa ili kuwahudumia, kuwafundisha na kuwaimarisha viongozi wa eneo husika, wamisionari na waumini wa Kanisa. Wanapangiwa na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kusimamia mikutano ya vigingi pamoja na mikutano mingineyo.”2

“Ofisi ya Sabini kwenye Ukuhani wa Melkizedeki inarejelewa kote kwenye Agano la Kale na Jipya,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla kinatueleza hivyo (ona kutoka 24:1, 9–10; Luka 10:1, 17). Hivi leo, kuna Sabini Wakuu wenye Mamlaka na Sabini wa Maeneo. Wanatenda chini ya funguo na maelekezo ya Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Wanawasaidia Kumi na Wawili katika kujenga na kuongoza Kanisa katika mataifa yote (ona Mafundisho na Maagano 107:34–35, 38).

Sabini Wakuu wenye Mamlaka wanatumikia kwa muda wote ndani ya Kanisa. Kiujumla wanapumzishwa katika mwaka ambao wanafikia miaka 70 na wanapewa cheo cha heshima. Ingawa wanabaki kwenye ofisi ya Sabini, hawaendelei tena kusimamia mikutano.”3

Ili kujifunza zaidi kuhusu Urais wa Maeneo, tazama Kitabu cha Maelezo ya Jumla:

Muhtasari

  1. General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 5.2, ChurchofJesusChrist.org.

  2. General Handbook, 5.2.1.

  3. General Handbook, 5.1.1.2.