Sehemu ya 129
Mafundisho yaliyotolewa na Joseph Smith Nabii, huko Nauvoo, Illinois, 9 Februari 1843, ambayo yanaelezea funguo kuu tatu ambazo kwa hizo twaweza kutofautisha aina sahihi za malaika na roho wahudumu.
1–3, Mbinguni kuna miili ya waliofufuka na miili ya kiroho; 4–9, Funguo zimetolewa ambazo kwa hizo wajumbe kutoka ngʼambo ya pazia wanaweza kutambulika.
1 Kuna viumbe wa aina mbili mbinguni, nao ni: Malaika, ambao ni watu waliofufuka, wenye miili ya nyama na mifupa—
2 Kwa mfano, Yesu alisema: Nishikenishikeni na mwone, kwa kuwa roho haina mwili na mifupa, kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.
3 Ya pili, ni roho za watu wenye haki waliokamilika, wale ambao hawajafufuka, lakini wanarithi utukufu huo huo
4 Wakati mjumbe akija akisema anao ujumbe kutoka kwa Mungu, mpe mkono wako na mwombe mshikane mikono.
5 Kama yeye atakuwa malaika atafanya hivyo, nawe utausikia mkono wake.
6 Kama atakuwa roho ya mtu mwenye haki aliyekamilika yeye atakuja katika utukufu wake; kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee anayoweza kuonekana—
7 Mwombe mshikane mikono, lakini yeye hatafanya lolote, kwa sababu ni kinyume cha utaratibu wa mbinguni kwa mtu mwenye haki kudanganya; lakini yeye bado atatoa ujumbe wake—
8 Lakini ikiwa ni ya ibilisi akiwa kama malaika wa nuru, ukimwomba kushikana mikono naye atakupa mkono wake, na wewe hutasikia chochote; nawe utaweza kumgundua.
9 Hizi ndizo funguo kuu tatu ambazo kwa njia hiyo ninyi mtaweza kujua iwapo huduma yoyote yatoka kwa Mungu.