Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 137


Sehemu ya 137

Ono lililotolewa kwa Joseph Smith Nabii, ndani ya hekalu huko Kirtland, Ohio, 21 Januari 1836. Tukio lilikuwa la huduma za ibada katika maandalizi kwa ajili ya uwekaji wakfu wa hekalu.

1–6, Nabii anamwona kaka yake Alvin katika ufalme wa selestia; 7–9, Mafundisho ya wokovu kwa ajili ya wafu yanafunuliwa; 10, Watoto wote wameokolewa katika ufalme wa selestia.

1 Mbingu zikatufunukia, nami nikauona ufalme wa selestia wa Mungu, na utukufu wake, kama nilikuwa katika mwili au nilikuwa nje ya mwili sijui.

2 Niliona uzuri uliopita kiasi wa lango ambalo warithi wa ufalme ule wataingia, ambalo lilikuwa mfano wa miale ya moto yenye kuzunguka;

3 Pia kiti cha enzi cha Mungu chenye kuwaka, juu yake Baba na Mwana wamekaa.

4 Niliona mitaa mizuri ya ufalme ule, ambayo ilionekana kuwa kama umesakafiwa kwa dhahabu.

5 Nilimwona Baba Adamu na Ibrahimu; na baba na mama yangu; kaka yangu Alvin, ambaye alifariki muda mrefu uliopita.

6 Na nikastaajabu jinsi gani ameweza kupata urithi katika ufalme ule, nilitazama kwamba ameondoka katika maisha haya kabla Bwana hajaweka mkono wake kuwakusanya Israeli mara ya pili, na wala hakubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi.

7 Na hivyo sauti ya Bwana ikanijia ikisema: Wote waliokufa bila kuifahamu injili hii, ambao wangeliipokea kama wangeruhusiwa kuishi, watakuwa warithi wa ufalme wa selestia wa Mungu;

8 Pia wale wote watakaokufa sasa na kuendelea bila kuifahamu, ambao wangeliipokea kwa moyo wao wote, watakuwa warithi wa ufalme huo;

9 Kwani Mimi, Bwana, nitawahukumu watu wote kulingana na matendo yao, kulingana na tamaa za mioyo yao.

10 Nami pia niliona kwamba watoto wote ambao hufa kabla ya kufikia miaka ya uwajibikaji wanaokolewa katika ufalme wa selestia wa mbinguni.