Misaada ya Kujifunza
Adamu


Adamu

Mwanadamu wa kwanza kuumbwa duniani.

Adamu ndiye baba na patriaki wa jamii ya wanadamu duniani. Uvunjaji wa sheria katika Bustani ya Edeni (Mwa. 3; M&M 29:40–42; Musa 4) ulimsababisha “aanguke” na kuwa mwenye kufa, hatua iliyo muhimu kwa mwanadamu kukua hapa duniani (2 Ne. 2:14–29; Alma 12:21–26). Kwa sababu hiyo Adamu na Hawa yapaswa waheshimiwe kwa kazi yao waliyofanya katika kuwezesha makuzi yetu ya milele. Adamu ndiye Mzee wa Siku na pia hujulikana kama Mikaeli (Dan. 7; M&M 27:11; 107:53–54; 116; 138:38). Yeye ndiye malaika mkuu (M&M 107:54) na atakuja tena duniani kama patriaki wa familia ya wanadamu, kama matayarisho kwa ujio wa pili wa Yesu Kristo (M&M 116).