Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 77


Sehemu ya 77

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii huko Hiram, Ohio, kama Machi 1832. Historia ya Joseph Smith inaeleza, “Kuhusiana na tafsiri, ya Maandiko, nilipokea ufafanuzi ufuatao wa Ufunuo wa Mt. Yohana.”

1–4, Wanyama wana roho na wataishi katika furaha ya milele juu ya dunia isiyo kufa; 5–7, Dunia hii itaishi kwa muda wa miaka 7000; 8–10, Malaika mbalimbali huirejesha injili na kuhudumu duniani; 11, Waliotiwa muhuri kwa 144,000; 12–14, Kristo atakuja mwanzoni mwa miaka ya elfu saba; 15, Manabii wawili watainuliwa kwa taifa la Israeli.

1 S. Bahari ya kioo iliyozungumzwa na Yohana, mlango 4 na mstari wa 6 wa Ufunuo ni nini?J. Ni dunia, katika hali yake ya kutakaswa, isiyokufa, na ya milele.

2 S. Tuelewe nini kwa wanyama wanne, waliozungumzwa katika mstari huo huo?J. Ni maneno ya ishara, yaliyotumiwa na Mfunuzi, Yohana, katika kueleza mbingu, peponi ya Mungu, furaha ya mwanandamu, na ya wanyama, na ya vitu vitambaavyo, na ya ndege wa angani; na kile kilicho kiumbe cha kiroho katika kufanana na kile kilicho cha kimwili; na kile kiumbe cha kimwili katika kufanana na kile cha kiroho; roho ya mwanadamu katika kufanana na mwili wake, vivyo hivyo pia roho ya mnyama, na kila kiumbe ambacho Mungu amekiumba.

3 S. Je, wanyama wale wanne inamaanisha wanawakilisha wanyama maalumu tu, au wanawakilisha wanyama mbalimbali?J. Wanawakilisha wanyama maalumu wanne, ambao walionyeshwa kwa Yohana, ili kuwakilisha utukufu wa makundi ya viumbe katika mpangilio wao uliokusudiwa au eneo la uumbaji, katika kufurahia furaha yao ya milele.

4 S. Tuelewe nini kwa macho na mabawa ambayo wanyama wale walikuwa nayo?J. Macho yao yanawakilisha nuru na maarifa, maana yake, wamejaa maarifa; na mabawa yao yanawakilisha uwezo, wa kutembea, wa kutenda, na kadhalika.

5 S. Tuelewe nini kwa wazee ishirini na wanne, waliozungumzwa na Yohana?J. Tuelewe kuwa wazee hawa aliowaona Yohana, walikuwa wazee waliokuwa waaminifu katika kazi ya huduma na walikufa; na walikuwa wa makanisa yale saba, na walikuwa katika peponi ya Mungu.

6 S. Tuelewe nini kwa kitabu ambacho Yohana alikiona, ambacho kilikuwa kimetiwa lakiri nyuma kwa lakiri saba?J. Tuelewe kuwa inajumuisha mapenzi yaliyofunuliwa, siri, na kazi za Mungu; mambo yake yaliyofichika ya utawala wake kuhusu dunia katika kipindi cha miaka elfu saba cha kudumu kwake, au katika uhai wake.

7 S. Tuelewe nini kwa lakiri saba zlizotiwa?J. Tuelewe kuwa muhuri wa kwanza ni juu ya mambo ya miaka elfu moja ya kwanza, na wa pili pia ni juu ya miaka elfu ya pili, na kuendelea hadi wa saba.

8 S. Tuelewe nini kwa malaika wanne, waliozungumzwa katika mlango wa 7 na mstari wa 1 wa Ufunuo?J. Tuelewe kuwa ni malaika wanne waliotumwa kutoka kwa Mungu, ambao wamepewa uwezo juu ya pembe nne za nchi, kuponya uhai au kuangamiza; hawa ndiyo wale wenye injili isiyo na mwisho ya kuhubiri kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu; wakiwa na uwezo wa kuzifunga mbingu, kuwafungia maisha, au kuwatupa chini sehemu ya giza.

9 S. Tuelewe nini kwa malaika kushuka kutoka mashariki, Ufunuo mlango wa 7 na mstari wa 2?J. Tuelewe kuwa malaika ashukaye kutoka mashariki ni yule aliyepewa muhuri wa Mungu aliye hai kwa ajili ya makabila kumi na mawili ya Israeli; kwa hiyo, akilia kwa malaika wanne wenye injili isiyo na mwisho, akisema: Msidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapo kwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Na, ikiwa mtaipokea, huyu ndiye Elia atakayekuja kuyakusanya pamoja makabila ya Israel na kurejesha mambo yote.

10 S. Mambo yaliyozungumzwa katika mlango huu yatamalizika wakati gani?J. Yatamalizika katika kipindi cha miaka elfu sita, au kufunguliwa kwa lakiri ya sita.

11 S. Tuelewe nini kwa kutiwa muhuri kwa watu mia moja na arobaini na nne elfu kutoka makabila yote ya Israeli—kumi na wawili elfu kutoka kila kabila?J. Tuelewe kuwa wale waliotiwa muhuri ni makuhani wakuu, waliotawazwa katika mpango mtakatifu wa Mungu! kusimamia injili isiyo na mwisho; kwani wao ndiyo waliotawazwa kutoka kila taifa, kabila, lugha, na watu, na malaika ambao walipewa uwezo juu ya mataifa ya dunia, kuwaleta wengi kadiri iwezekanavyo katika kanisa la Mzaliwa wa Kwanza.

12 S. Tuelewe nini kwa kupigwa kwa mabaragumu, yaliyotajwa katika mlango wa 8 wa Ufunuo?J. Tuelewe kuwa kama vile Mungu alivyoumba ulimwengu katika siku sita, na siku ya saba akamaliza kazi yake, na akaitakasa, na pia akamtengeneza mwanadamu kutoka mavumbi ya dunia, hata hivyo, mwanzoni mwa miaka elfu saba Bwana Mungu ataitakasa dunia, na kukamilisha wokovu wa mwanadamu, na kuvihukumu vitu vyote, na atavikomboa vitu vyote, isipokuwa kile ambacho hakukiweka ndani ya uwezo wake, wakati atakapokuwa amekwisha tia muhuri vitu vyote, hata mwisho wa vitu vyote; na kupigwa kwa parapanda za malaika saba ni kutayarisha na kumalizika kwa kazi yake, mwanzoni mwa miaka ya elfu saba—kutayarisha njia kabla ya wakati wa kuja kwake.

13 S. Ni lini yatatimizwa mambo yaliyoandikwa katika mlango wa 9 wa Ufunuo?J. Yatatimizwa baada ya kufunguliwa kwa lakiri ya saba, kabla ya kuja kwa Kristo.

14 S. Tuelewe nini kwa kitabu kidogo kilicholiwa na Yohana, kama ilivyotajwa katika mlango wa 10 wa Ufunuo?J. Tuelewe kuwa ilikuwa ni kazi na ibada, kwake yeye ya kuyakusanya makabila ya Israeli; tazama, huyu ndiye Elia, ambaye, kama ilivyoandikwa, ni lazima atakuja naye atarejesha mambo yote.

15 S. Nini kieleweke kwa mashahidi wawili, katika mlango wa kumi na moja ya Ufunuo?J. Ieleweke kuwa ni manabii wawili ambao watainuliwa kwa taifa la Kiyahudi katika siku za mwisho, wakati wa urejesho, na wa kutoa unabii kwa Wayahudi baada ya kukusanywa na kujenga mji wa Yerusalemu katika nchi ya baba zao.